Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Muungano wa nchi ya Kiarabu washushia lawama waasi wa Houthi kuhusika na vifo vya raia

Muungano wa nchi zinazoongozwa na Saudi Arabia kupambana na waasi wa Houthi nchini Yemen, umekukanusha ripoti za kuhusika na shambulizi la angaa katika ngome ya waasi, Kaskazini mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya rais 70 wakiwemo, wahamiaji, wanawake na watoto.

Ramani inayoonesha mji mkuu wa Yemen, Sana'a.
Ramani inayoonesha mji mkuu wa Yemen, Sana'a. AFP
Matangazo ya kibiashara

Badala yake muungano huo wa jeshi unawashtumu waasi hao kuhusika, na hii inakuja baada ya waasi hao kuhusika na shambulizi katika kituo cha mafuta mjini Abu Dhabi, siku ya Jumatatu katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu. 

Antonio Guteress ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mauaji ya raia na kutaka uchunguzi kufanyika. 

Shambulizi lolote linalolenga raia halikubaliki, tunastahili kuachana na mzunguko huu, na kitu ambacho tunapendekeza na tumekuwa tukipendekeza kila mara ni kuwa, kuwe na usitishwaji wa vita na kufunguliwa kwa bandari, viwanja vya ndege na pande zote zizungumze, kuendelea kwa mivutano mashambulizi kunapaswa kufika mwisho. 
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.