Pata taarifa kuu
MAHAKAMA-MAANDAMANO

Israeli: Benjamin Netanyahu atangaza 'kusitishwa' mageuzi ya mahakama

Waziri Mkuu wa Israel ametangaza Jumatatu Machi 27 'kusitisha' mradi wenye utata wa mageuzi ya mfumo wa mahakama ambao umezusha mvutano, maandamano na mgomo wa jumla nchini humo. Chama kikuu cha wafanyakazi kimetangaza mara moja kumalizika kwa mgomo wa jumla.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiondoka 10 Downing Street baada ya mkutano na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak mjini London, Ijumaa, Machi 24, 2023.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiondoka 10 Downing Street baada ya mkutano na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak mjini London, Ijumaa, Machi 24, 2023. © AP - Alberto Pezzali
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amelihutubia taifa baada ya mashauriano ya kisiasa na baadhi ya washirika wa muungano tawala. Kiongozi huyo wa Israel ametangaza kwamba upitishwaji wa mwisho wa miswada mbalimbali ya mageuzi umeahirishwa hadi kikao kijacho cha bunge kitakachofunguliwa baada ya sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi (Aprili 5 hadi 13), na hivyo kukubaliana na matakwa ya wapinzani.

'Kuepukana na mpasuko wa taifa'

Ameelezea uamuzi wake kwa "nia ya kuepusha kusambaratika kwa taifa" na kuwa na wakati wa "kufikia makubaliano mapana" juu ya mageuzi ya mfumo wa maakama, hali ambayo ameelezea hapo awali kuwa inawajibika na muhimu kwa kusawazisha tena madaraka katika Israeli.

Mradi huo unaolaaniwa na wapinzani kuwa ni kikwazo kwa demokrasia, unalenga kuipa serikali uzito mkubwa katika uchaguzi wa majaji na kupunguza uwezo wa Mahakama ya Juu kubatilisha sheria zilizopitishwa na Bunge.

Kwa kuguswa na tangazo la kuahirishwa kwa mswada huo, Histadrut, chama kikuu cha wafanyakazi nchini, kimetangaza kumalizika kwa mgomo wa jumla uliozinduliwa asubuhi ili kuzuia mageuzi ya mfumo wa mahakama ambayo yamekuwa yakipingwa kwa karibu miezi mitatu kwa maandamano. "Kufuatia tangazo la Waziri Mkuu, ninatangaza kumalizika kwa mgomo [...] uliotangazwa leo asubuhi," kiongozi wa Histadrut, Arnon Bar David, amesema katika taarifa.

Maandamano makubwa

Muswada huo ulizusha maandamano makubwa ya umma, yaliyoashiriwa na maandamano ya kila wiki ya kuwaleta pamoja maelfu kadhaa ya Waisraeli katika miji mikubwa ya nchi hiyo.

Kabla ya hotuba ya runinga ya Benjamin Netanyahu, Waziri wa Usalama wa Kitaifa Itamar Ben-Gvir kwa mara nyingine ameelezea upinzani wake wa kusitiishwa kwa mageuzi siku ya Jumatatu. "Hatupaswi kusitisha mageuzi ya mfumo wa mahakama na tusikubali machafuko," amesema kwenye Twitter.

Kusoma pia: Netanyahu amfukuza kazi waziri wake wa ulinzi na kusababisha sintofahamu ya kisiasa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.