Pata taarifa kuu

Israel: Netanyahu amfukuza kazi waziri wake wa ulinzi na kusababisha sintofahamu ya kisiasa

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant alifutwa kazi siku ya Jumapili Machi 26. Alikuwa amependekeza Jumamosi jioni kusitishwa kwa mageuzi ya mfumo wa mahakama ambayo, machoni pake, yanawasilisha hatari za wazi na za haraka kwa nchi.

Waziri Mkuu wa Israel Binyamin Netanyahu na Waziri wake wa zamani wa Ulinzi Yoav Gallant.
Waziri Mkuu wa Israel Binyamin Netanyahu na Waziri wake wa zamani wa Ulinzi Yoav Gallant. © GALI TIBBON / AFP / POOL
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa serikali, Benyamin Netanyahu, kwa hivyo anaunga mkono wazi mrengo wa kulia wa muungano wake. Hayo yanajiri wakati balozi mdogo wa Israel mjini New York ametangaza kujiuzulu.

Na mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul

Majibu ya upinzani wa Israel ni makubwa mno. Muungano huo unapinga Uzayuni, anasema Yair Lapid, kiongozi wa upinzani. Benjamin Netanyahu anahatarisha nchi, ameongeza. Bw Netanyahu amegeuza serikali yake kuwa nyumba ya webdawazimu, kiongozi mwingine wa upinzani amesema.

Waziri Mkuu wa Israel alifanya uchaguzi wake haraka kuliko ilivyotarajiwa. Chini ya saa 24 baada ya wito wa mazungumzo na kusimamishwa kwa mwezi mmoja kwa mageuzi ya mahakama hatu iliyochukuliwa na Yoav Gallant, Waziri mkuu ameamua kuchukuwa uamuzi wa kumfuta kazi Waziri wake wa Ulinzi baada ya mazungumzo yao mafupi.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, mkuu wa serikali ya Israel anadai kuwa amepoteza imani yake kwa Bw. Gallant, ambaye alichukuwa hatua bila kushauriana naye alipokuwa akisafiri nje ya nchi.

Muungano wenye msimamo mkali unaotawala nchini Israel unakaribisha uamuzi huu. Na Knesset, Bunge la Israeli, litaendelea kupiga kura kwa mageuzi hayo katika siku zijazo. Waziri aliyeondolewa ambaye anaendelea kuwa mbunge, hakuonyesha iwapo alinuia kupinga mradi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.