Pata taarifa kuu

Israel: Benyamin Netanyahu aidhinisha ombi la msaada kwa Syria baada ya tetemeko la ardhi

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametangaza siku ya Jumatatu kwamba 'ameidhinisha' kutumwa kwa msaada nchini Syria, iliyokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi, baada ya ombi kutoka Damascus kupokelewa kupitia njia za "kidiplomasia", nchi hizo mbili hazina uhusiano wowote rasmi.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. AFP - RONEN ZVULUN
Matangazo ya kibiashara

Israel "imepokea ombi kutoka kwa chanzo cha kidiplomasia kwa msaada wa kibinadamu nchini Syria na nimeidhinisha," Benjamin Netanyahu amewaambia wabunge wa chama chake, Likud. Msaada utatumwa hivi karibuni, amesema.

Watu zaidi ya Elfu Mbili wameripotiwa kupoteza maisha Kusini mwa Uturuki na Kaskazini mwa Syria, baada ya kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa ritcha 7.8, wakati huu mataifa mbalimbali ya dunia yakijitokeza kutuma misaada ya kibinadamu na watu zaidi wakitafutwa.

Tetemeko hilo liliathiri sehemu zote za miji mikubwa ya Uturuki katika eneo lililojaa mamilioni ya watu, waliokimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria na maeneo mengine ya migogoro.

Mkuu wa Kituo cha Kitaifa cha Matetemeko ya Ardhi nchini Syria, Raed Ahmed, aliiambia redio ya taifa kwamba hilo lilikuwa tetemeko kubwa zaidi, kuwahi kurekodiwa katika historia nchini Uturuki

Serikali imelazimika kukata nguvu za umeme na gesi katika eneo lote kwa wiki mbili ili kupunguza athari na maafa zaidi.

Uturuki ni mojawapo ya mataifa ambayo yako katika maeneo yenye tetemeko la ardhi duniani.

Wataalam wameonya kwa muda mrefu kwamba tetemeko kubwa linaweza kutokea na kuharibu mji wa Istanbul, ambao una wakaazi milioni 16.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.