Pata taarifa kuu
SYRIA - UTURUKI MTETEMEKO WA ARDHI

Uturuki/Syria: Watu zaidi ya elfu mbili wamefariki katika tetemeko la ardhi

Watu zaidi ya Elfu Mbili wameripotiwa kupoteza maisha Kusini mwa Uturuki na Kaskazini mwa Syria, baada ya kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa ritcha 7.8, wakati huu mataifa mbalimbali ya dunia yakijitokeza kutuma misaada ya kibinadamu na watu zaidi wakitafutwa.

Zaidi ya watu elfu mbili wamefariki katika mtetemeko wa ardhi nchini Uturuki na Syria
Zaidi ya watu elfu mbili wamefariki katika mtetemeko wa ardhi nchini Uturuki na Syria © AP - Mahmut Bozarslan
Matangazo ya kibiashara

Tetemeko hilo liliathiri sehemu zote za miji mikubwa ya Uturuki katika eneo lililojaa mamilioni ya watu, waliokimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria na maeneo mengine ya migogoro.

Mkuu wa Kituo cha Kitaifa cha Matetemeko ya Ardhi nchini Syria, Raed Ahmed, aliiambia redio ya taifa kwamba hilo lilikuwa tetemeko kubwa zaidi, kuwahi kurekodiwa katika historia nchini Uturuki

Serikali imelazimika kukata nguvu za umeme na gesi katika eneo lote kwa wiki mbili ili kupunguza athari na maafa zaidi.

Uturuki ni mojawapo ya mataifa ambayo yako katika maeneo yenye tetemeko la ardhi duniani.

Wataalam wameonya kwa muda mrefu kwamba tetemeko kubwa linaweza kutokea na kuharibu mji wa Istanbul, ambao una wakaazi milioni 16.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.