Pata taarifa kuu

Isareli: Raia waandamana kupinga kufutwa kazi kwa Waziri wa Ulinzi

NAIROBI – Maelfu ya raia wa Israeli wameendamana dhidi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, baada ya kumfuta kazi Waziri wake wa Ulinzi, aliyeitaka serikali kuachana na mpango tata wa kuifanyia mageuzi idara ya Mahakama. 

Raia wa Israeli wamekuwa wakiandamana kupinga mageuzi yanayopendekezwa katika idara ya mahakama
Raia wa Israeli wamekuwa wakiandamana kupinga mageuzi yanayopendekezwa katika idara ya mahakama © REUTERS / OREN ALON
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji walifunga barabara kuu jijini Tel Aviv' huku wengine wakiwasha moto kuonesha hasira yao, baada ya uamuzi wa Netanyahu kumwachisha kazi Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant kwa msimamo wake. 

Inaelezwa kuwa waandamanaji zaidi ya Laki mbili, walijitokeza kupinga mageuzi hayo na kufutwa kazi kwa Waziri huyo, wakisema mchakato huo wa Mahakama ni lazima ukomeshwe kwa sababu unaigawa nchi. 

Miongoni mwa mabadiliko hayo, ni kutoa kipaumbele kwa wanasiasa na serikali, kuunda Kamati itakayowateuwa Majaji wa Mahakama. 

Hatua hiyo pia imesababisha kujiuzulu kwa Asaf Zamir, mwanadiplomasia wa Israeli jijini New York, ambaye amesema hawezi kuendelea kuiwakilisha serikai hiyo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.