Pata taarifa kuu
MVUTANO-SIASA

Hali ya wasiwasi yatanda nchini Israel kufuatia mpango wa mageuzi ya mfumo wa mahakama

Muungano mkuu wa vyama vya wafanyakazi nchini Israel umetangaza leo Jumatatu 'mgomo wa jumla wa haraka', ukitaka kusitishwa kwa mradi wa mageuzi ya mfumo wa mahakama ambao unaigawanya nchi hiyo, ikielekea kwenye mgogoro mpya wa kisiasa.

Polisi wa Israel wakiwatawanya waandamanaji wanaofunga barabara kuu wakati wa maandamano dhidi ya mpango wa serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa kurekebisha mfumo wa mahakama huko Tel Aviv, Israel, Jumatatu, Machi 27, 2023. Makumi kwa maelfu ya Waisraeli wamemiminika mitaani kote nchini humo. hasira ya ghafla baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kumfukuza kazi waziri wake wa ulinzi kwa kupinga mpango wa marekebisho ya mahakama ya kiongozi huyo wa Israel.
Polisi wa Israel wakiwatawanya waandamanaji wanaofunga barabara kuu wakati wa maandamano dhidi ya mpango wa serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa kurekebisha mfumo wa mahakama huko Tel Aviv, Israel, Jumatatu, Machi 27, 2023. Makumi kwa maelfu ya Waisraeli wamemiminika mitaani kote nchini humo. hasira ya ghafla baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kumfukuza kazi waziri wake wa ulinzi kwa kupinga mpango wa marekebisho ya mahakama ya kiongozi huyo wa Israel. © Oren Ziv / AP
Matangazo ya kibiashara

Saa sita mchana, nchi hiyo imeachana na tangazo la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, ambalo limeripotiwa kuwa ni hatari na vyombo vya habari vya Israeli tangu asubuhi juu ya mradi huu, ambao sasa unadhoofisha walio wengi.

Kabla ya hili, Arnon Bar David, kiongozi wa muungano wa vyama vya wafanyakazi, Histadrut, alikuwa ameitisha mgomo wa jumla. "Mara tu mkutano huu wa waandishi wa habari unapomalizika, Taifa la Israel linasimama. Tuna dhamira ya kusitisha mchakato wa kutunga sheria na hilo tutalifanya," amesema. Chama cha Madaktari nchini Israeli pia kimetangaza mgomo wa jumla ambao utaathiri hospitali za umma na idara ya huduma za matibabu.

Iwapo madhara ya mgomo huo si lazima yaonekane mara moja katika mitaa ya Jerusalem au Tel Aviv, ambako biashara nyingi zimesalia wazi, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ben-Gurion umetangaza kusitisha safari za ndege za kuondoka huku makumi ya maelfu ya watu walikuwa wanajiandaa kuondoka nchini leo Jumatatu.

"Mageuzi yasiyo kuwa na busara"

Saa saba kamili mchana, maelfu ya wapinzani wa mageuzi wameandamana mbele ya Bunge mjini Jerusalem, kulingana na waandishi wa habari wa AFP waliopo eneo hilo. Maandamano ya kama hayo yamepangwa jioni. Maandamano ya kupinga mageuzi ya mfumo wa mahakama pia yanafanyika Haifa na Tel Aviv.

"Tunatoa wito kwa serikali kukomesha mageuzi haya yasiyo na maana, tunataka usawa, Katiba na tamko la haki za binadamu," Keren Mimran, 57, ameliambia shirika la habari la AFP, ambaye alikuja kupinga mageuzi hayo mbele ya Bunge.

Mapema asubuhi, Rais Isaac Herzog alitoa wito kwa serikali "kusitisha mara moja" kazi ya kutunga sheria kuhusu mswada wa marekebisho ya mahakama, baada ya usiku uliokumbwa na makabiliano kati ya waandamanaji na polisi mjini Tel Aviv.

Bw. Herzog ana jukumu la kimsingi la sherehe na wito wake wa mara kwa mara wa kutafuta suluhu la maafikiano juu ya mageuzi hadi sasa haujatekelezwa na haujaizuia nchi hiyo kutumbukia hatua kwa hatua kwenye mgogoro. Hivi karibuni alikuwa na wasiwasi juu ya hatari ya "vita vya wenyewe kwa wenyewe".

Lakini kulingana na vyombo vya habari vya Israel, Netanyahu anaweza kutangaza kusitisha mageuzi, sambamba na wito huo. Maelfu ya watu waliingia barabarani mjini Tel Aviv Jumapili jioni baada ya Bw Netanyahu kumfukuza kazi waziri wake wa ulinzi, Yoav Gallant, ambaye alikuwa ameomba hadharani siku moja kabla, kusitisha mageuzi hayo, akionyesha hofu kwa usalama wa Israeli.

Mradi wa mageuzi uliopendekezwa na serikali ya Bw. Netanyahu, mojawapo ya mrengo wa kulia zaidi katika historia ya Israel, unalenga kuongeza mamlaka ya viongozi waliochaguliwa kuliko majaji. Akiwa anapigwa mtaani kwa karibu miezi mitatu, yuko kwenye chimbuko la vuguvugu kubwa zaidi la uhamasishaji katika historia ya Israeli.

'Maelewano'

Wakosoaji wa mageuzi hayo wanaamini kwamba inaweza kuhatarisha tabia ya kidemokrasia ya taifa la Israeli. Lakini, ishara kwamba mchakato wa kutunga sheria bado haujasitishwa, Tume ya Sheria ya Bunge ilipiga kura Jumatatu asubuhi kuunga mkono moja ya vipengele muhimu vya mageuzi hayo, katika kiini cha wasiwasi wa wapinzani wake muswada wa kurekebisha mchakato wa uteuzi wa majaji.

Marekani ambayo ni mshirika mkuu wa Israel, imetangaza kuwa inatiwa wasuwasi na hali hiyo na kubaini "haja ya haraka ya maelewano". Nchini Ufaransa, nchi ambayo Wayahudi wengi zaidi wanaishi baada ya Israel na Marekani, Baraza linalowakilisha Taasisi za Kiyahudi la Ufaransa (Crif) limeitaka serikali ya Israel "kusitisha mageuzi hayo" ili "kurejesha utulivu na mazungumzo na jamii nzima".

"Natoa wito kwa Waziri Mkuu kubatilisha uamuzi wa kumfuta kazi Yoav Gallant. Taifa la Israel haliwezi kwa wakati huu, licha ya vitisho vya pande zote, kuruhusu mabadiliko ya Waziri wa Ulinzi," amesema kwa upande wake kiongozi wa upinzani nchini Israel Yaïr Lapid, katika mkutano na waandishi wa habari, aliungana kwa maana hii na Yuli Edelstein, kiongozi wa Likud, chama cha Bw. Netanyahu.

"Kwa kuzingatia hali ya usalama, ni dhahiri kwamba huu sio wakati wa kubadilisha waziri wa ulinzi," amesema Bw. Edelstein, mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mashauri ya kigeni na ulinzi.

Wakati vyombo vya habari vya Israel vikiibua tishio kutoka kwa Waziri wa Usalama wa Ndani, Itamar Ben Gvir, kuondoka serikalini jambo ambalo linaweza kumfanya Bwana Netanyahu kupoteza wingi wake katika tukio la kusitishwa kwa mageuzi hayo, Waziri wa Uchumi, Nir Barkat, kiongozi mwingine wa chama cha Likud, ametoa wito kwa wenzake kwenye Twitter "kumuunga mkono waziri mkuu kufanikisha mageuzi haya ya mfumo wa mahakama".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.