Pata taarifa kuu

Mgogoro wa kiuchumi: Lebanon inapitia 'wakati hatari', IMF yaonya

Lebanon ilifikia makubaliano muhimu na Shirika la fedha la Kimataifa, IMF, mnamo mwezi Aprili 2022, lakini itafanya mageuzi muhimu ya kufungua misaada ili kufufua uchumi wa nchi, ambapo zaidi ya 80% ya watu sasa wanaishi chini ya mstari wa umaskini, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Maandamano dhidi ya kuzorota kwa hali ya uchumi, katika eeo la Riad al-Solh huko Beirut, Lebanon, Machi 22, 2023.
Maandamano dhidi ya kuzorota kwa hali ya uchumi, katika eeo la Riad al-Solh huko Beirut, Lebanon, Machi 22, 2023. REUTERS - MOHAMED AZAKIR
Matangazo ya kibiashara

Lebanon, ambako mzozo wa kiuchumi unazidi kuwa mbaya siku baada ya siku, inapitia 'wakati hatari', afisa wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ameonya siku ya Alhamisi, akisikitishwa na ucheleweshaji wa utekelezaji wa mageuzi unaofanywa na viongozi wa kisiasa. Ernesto Ramirez Rigo amemaliza misheni kwenda Beirut, ambapo alikutana na maafisa kadhaa pamoja na wanadiplomasia.

"Mchakato wa kutekeleza" mageuzi muhimu "umekuwa wa polepole sana," afisa huyo aliongeza. "Tuko katika hali ambayo hali iliyopo [...] na sera ya kutochukua hatua itaiacha Lebanoni kutumbukia katika mgogoro usioisha. »

Makubaliano hayo kimsingi, yaliyohitimishwa mwezi Aprili 2022 na IMF, yanahusu msaada wa dola bilioni tatu, uliopangiliwa kwa miaka minne, lakini unaendana na masharti ya utekelezaji wa mageuzi, ikiwa ni pamoja na marekebisho ya sheria kuhusu usiri wa benki au marekebisho katika sekta ya benki, pamoja na sheria ya udhibiti wa mitaji.

"Muda unakwenda, ni takriban mwaka mmoja tangu tufikie makubaliano," amesema Ernesto Ramirez Rigo. Walebanon wamepiga hatua, lakini kwa bahati mbaya maendeleo haya yanakwenda kwa mwendo wa kinyonga."

Hii si mara ya kwanza kwa Mfuko huo kushutumu ucheleweshaji wa mamlaka ya Lebanon katika kutekeleza mageuzi haya, wakati nchi hiyo inakabiliwa na moja ya migogoro mibaya zaidi ya kiuchumi duniani tangu mwaka 1850, kulingana na Benki ya Dunia. Tangu mwaka 2019, Lebanon imetumbukia katika mzozo mkubwa wa kiuchumi unaolaumiwa na sehemu kubwa ya idadi ya watu juu ya usimamizi mbaya, ufisadi, uzembe na kushindwa kwajamii inayotawala kwa miongo kadhaa.

Mgogoro wa kisiasa usosaidia chochote

Mgogoro wa kisiasa nchini Lebanon unazidisha hali hiyo kuwa mbaya, wakati wabunge wameshindwa kukubaliana kumchagua rais mpya wa Jamhuri tangu mwezi Novemba. Nchi inaongozwa na serikali iliyojiuzulu yenye mamlaka yaliyopunguzwa.

Sarafu ya nchi hiyo imepoteza zaidi ya 98% ya thamani yake dhidi ya dola katika soko sambamba, wakati vikwazo vikali vya benki vinazuia waokoaji kupata pesa zao bila malipo. Kama hali ilivyo itaendelea, nchi inaweza kukabiliwa" na mfumuko wa bei katika hali mbaya zaidi", alionya mkuu wa IMF.

Miongoni mwa masuala nyeti zaidi ni mgawanyo wa hasara katika sekta ya benki. Akirejelea "kiwango cha hasara kwa nchi ndogo kama Lebanon", Bw. Ramirez Rigo amekadiria kuwa "itabidi zigawanywe kati ya kila mtu [...] serikali, benki na waokoaji". Hata hivyo, alidokeza kuwa “waokoaji wadogo ndio wameathirika zaidi na janga [...] Wanateseka zaidi kuliko inavyopaswa. Walebanon wengi hawana uwezo wa kufikia akiba zao, ambazo zimezuiwa katika benki tangu mwaka 2019.

Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.