Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-UCHUMI

Waokoaji wenye hasira wa Lebanon waandamana na kuharibu benki

Mamia ya waokoaji wamevunja madirisha ya benki na kuchoma moto matairi siku ya Alhamisi huko Beirut kudai pesa zao zilizozuiliwa, kulingana na wapiga picha wa shirika la habari la AFP, huku sarafu ya Lebanon ikishuka kwa kasi dhidi ya dola.

Bunge la Lebanon limekuwa likikaliwa na wabunge wa upinzani tangu Januari 20, 2023 kudai kuchaguliwa kwa rais mpya.
Bunge la Lebanon limekuwa likikaliwa na wabunge wa upinzani tangu Januari 20, 2023 kudai kuchaguliwa kwa rais mpya. © Firas Hamdan/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika wilaya ya Badaro huko Beirut, takriban watu hamsini waliharibu kuta za benki angalau nne na kuchoma matairi mbele ya benki hizo, wakati wa maandamano yaliyoitishwa na chama cha waokoaji. Waandamanaji kisha walikusanyika mbele ya nyumba ya mfanyakazi wa benki katika viunga vya Beirut, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Tangu kuanza kwa mzozo wa kiuchumi ambao haujawahi kutokea mnamo 2019, pauni ya Lebanon imepoteza zaidi ya 95% ya thamani yake dhidi ya dola. Waokoaji hawaezi tena kufiki au kutoa akiba zao zilizozuiwa katika benki, hali ambayo imezuia uondoaji na uhamishaji wa pesa.

Mwaka jana, mfululizo wa wizi wa wateja wanaotaka kutoa akiba zao ulilazimisha benki kufunga kwa kiasi kwa wiki kadhaa. Mnamo Februari 6, Chama cha Benki nchini Lebanon (ABL) kilitangaza mgomo wa wazi katika sekta hiyo. 

"Miaka mitatu iliyopita waliiba pesa zetu," mmoja wa waandamanaji, Pascal al-Rassi, ameliambia shirika la habari la AFP. "Watu wengine hapa ni mamilionea lakini hawana hata senti mfukoni," anaendelea daktari huyu, akiwa amedhamiria kuandamana mpaka arudishiwe pesa zake.

Pauni imekuwa ikiuzwa kwa karibu 80,000 LL kwa dola moja siku ya Alhamisi, kulingana na tovuti za ufuatiliaji wa viwango vya ubadilishaji na wafanyabiashara, wakati mapema mwezi Februari ilikuwa ikiuzwa karibu 60,000 LL kwa dola moja. Anguko hili jipya limesababisha kupanda kwa bei ya bidhaa za kimsingi, katika nchi ambayo zaidi ya 80% ya raia wanaishi chini ya mstari wa umaskini, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Siku ya Jumatano, katika kukabiliana na kuzorota kwa hali zao za maisha, madereva kadhaa wa teksi walifunga barabara mbele ya Wizara ya Mambo ya Ndani mjini Beirut kupinga kushuka kwa mapato yao.

Lebanon inakabiliwa na moja ya migogoro mibaya zaidi ya kiuchumi duniani tangu 1850, kulingana na Benki ya Dunia, na upungufu wa umeme unafanya hali kuwa mbaya zaidi. Tangu Novemba 1, bunge lililogawanyika limeshindwa kumchagua rais mara kumi na moja. Nchi inatawaliwa na serikali ya mpito ambayo haiwezi kupitisha mageuzi yanayohitajika ili kupata misaada kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.