Pata taarifa kuu
UBADHIRIFU-HAKI

Ujumbe wa majaji wa Ulaya mjini Beirut kuchunguza ubadhirifu wa fedha

Zaidi ya miaka mitatu baada ya kuanza kwa vuguvugu la maandamano dhidi ya wanasiasa, hakuna maendeleo yoyote yaliyopatikana katika vita dhidi ya ufisadi nchini Lebanon. 

Mkuu wa Benki Kuu ya Lebanon Riad Salamé, wakati wa mahojiano yake na shirika la habari la AFP, Desemba 20, 2021.
Mkuu wa Benki Kuu ya Lebanon Riad Salamé, wakati wa mahojiano yake na shirika la habari la AFP, Desemba 20, 2021. AFP - JOSEPH EID
Matangazo ya kibiashara

Hakuna kiongozi mkuu aliyefunguliwa mashitaka, hakuna uchunguzi uliofanyika. Miongoni mwa watu wenye utata ni mkuu wa benki kuu ya Liban. Riad Salamé anachunguzwa katika nchi kadhaa za Ulaya kwa ubadhirifu, utajiri haramu na utakatishaji fedha unaohusisha kiasi cha dola milioni 330. Nchini Ufaransa, mpenzi wake wa zamani na mama wa mtoto wake, Anna Kosavoka, alishtakiwa msimu wa joto uliopita.

Ujumbe wa majaji kutoka Ufaransa, Ujerumani na Luxembourg unatarajiwa Jumatatu hii, Januari 9 mjini Beirut kuchunguza ubadhirifu wa fedha ambapo viongozi wakuu wa Lebanon wanadaiwa kuhusika. 

Majaji wa Ulaya wanatarajiwa kusikiliza takriban watu 25, akiwemo Riad Salamé na kaka yake Raja, ambao tayari wanafunguliwa mashitaka nchini Lebanon. Mashtaka ambayo pia yameshindwa kwa sababu ya kuingiliwa kisiasa katika mkondo wa haki. Majaji wa Ufaransa, Ujerumani na Luxembourg pia watakusanya taarifa za wamiliki na maafisa wakuu wa benki kadhaa zinazowasiliana kwa karibu na Benki Kuu ya Lebanon.

Kuingilia kati kwa majaji wa Ulaya kwazua mgawanyiko

Ujumbe wa Ulaya unaundwa na waendesha mashtaka wa umma, majaji wanaochunguza na waendesha mashtaka wa kifedha. Mahojiano yatafanyika mbele ya mahakimu wa Lebanon. Majaji hao pia ndio watawauliza watu walioitishwa maswali ya wachunguzi wa Ulaya. Watu ambao majaji wa Ulaya wanataka kuwasikiliza hawako katika hatari kubwa. Vyombo vya sheria vya Lebanon pia vimekataa kutoa hati za kukamatwa kwa watu ambao mahakimu wa Ulaya wanataka kuwauliza. Kwa hiyo, watu hawa wako huru kupokea au kukataa wito huo, kwa vile hawatakiwi kujibu maswali yote ambayo wataulizwa na wachunguzi katika tukio ambalo wamekubali kuhudhuria.

Kulingana na chanzo cha mahakama cha Lebanon, Riad Salamé bado hajaweka wazi nia yake. Wala kaka yake Raja. Jaji huyo alikamatwa mwaka jana kwa siku kadhaa kwa agizo la jaji wa kupambana na ufisadi nchini Lebanon Ghada Aoun, kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ya dola milioni 3.7.

Walebanon walio wengi wanafahamu kuwa rushwa ni tatizo kubwa nchini humo. Hata hivyo, ziara ya wajumbe wa mahakama ya Ulaya mjini Beirut iliibua hisia zinazokinzana kwenye vyombo vya habari na katika duru za mahakama na kisiasa. Baadhi wanachukulia uingiliaji kati wa majaji wa Ulaya kuwa halali, kwa vile Lebanon imetia saini Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Ufisadi tangu 2009. Hii inabainisha kuwa nchi iliyoidhinishwa inaweza kuomba usaidizi kutoka kwa nchi nyingine iliyotia saini, ili "kukusanya ushuhuda au amana" au "kupata hati asili au nakala zilizoidhinishwa za hati na faili".

Shambulio dhidi ya uhuru wa serikali?

Wengine, kwa upande mwingine, wanabaini kwamba mtazamo wa Ulaya unajumuisha shambulio dhidi ya uhuru wa Lebanon, hata udhalilishaji. Wanathibitisha kwamba vyombo vya sheria vya kigeni havipaswi kuchunguza "kwa uhuru" wa vyombo vya sheria vya Lebanon katika ardhi ya Lebanon. Mgawanyiko huo unaonekana kwenye mitandao ya kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.