Pata taarifa kuu
JAMII-UCHUMI

Mji mkuu wa Lebanon, Beirut, miongoni mwa miji mibaya zaidi katika suala la ubora wa maisha

Zaidi ya miaka mitatu baada ya kuzuka kwa mzozo wa kiuchumi, mnamo mwezi Oktoba 2019, Lebanon bado inakabiliwa na maisha magumu, huku hali ya kimaisha kwa Walebanon ikiendelea kuzorota. Bei zinapanda kila kukicha, mfumuko wa bei unapanda kwa kasi, Pauni ya Lebanon imeendelea kupoteza thamani yake. Kulingana na Benki ya Dunia, zaidi ya 80% ya raia wanaishi katika umaskini.

Ripoti ya kimataifa iliyochapishwa hivi karibuni inaonyesha kuwa mji mkuu wa Lebanon unatoa moja ya maisha magumu zaidi duniani.
Ripoti ya kimataifa iliyochapishwa hivi karibuni inaonyesha kuwa mji mkuu wa Lebanon unatoa moja ya maisha magumu zaidi duniani. © Gavin Hellier / GettyImages
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na ripoti ya kimataifa iliyochapishwa hivi karibuni inaonyesha kuwa mji mkuu wa Lebanon unatoa moja ya maisha magumu zaidi duniani. Ripoti ya hivi punde iliyotolewa na shirika la Numbeo inaiweka Beirut katika nafasi ya 240 kati ya miji 242 iliyoorodheshwa mwaka huu na hifadhidata hii. Takwimu zilizotolewa na utafiti huu zinaonyesha kwamba kuzorota kwa kiasi kikubwa na kwa ghafla kwa Lebanon kumekuwa na athari kubwa katika ubora wa maisha huko Beirut, ambayo wakati mmoja ilikuwa maarufu kwa kiwango cha huduma zinazotolewa.

Beirut sio tena jiji hili ambalo maisha yalikuwa mazuri. Bei zote zimeongezeka: 170% kwa chakula, 180% kwa usafiri. Gharama ya nyumba, ambayo ni pamoja na bei ya maji, gesi na umeme, imeongezeka hadi 235%. Elimu imepanda kwa 190% na mawasiliano ya simu 226%.

Ongezeko hili la gharama za maisha linaambatana na mporomoko mkubwa wa uwezo wa ununuzi kutokana na kushuka kwa thamani ya pauni ya Lebanon ambayo imepoteza asilimia 95 ya thamani yake dhidi ya dola. Mshahara wa chini, ambao ulikuwa sawa na dola 450 kabla ya mgogoro, kwa sasa ni dola 20.

Chanzo cha bunge kimeiambia RFI kuwa tangu mwezi Mei mwaka jana, watu 240,000 wametoroka nchi. Leila Dagher, profesa wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Marekani jijini Beirut anabaini katika ripoti juu ya athari za mzozo kwamba 78% ya wafanyakazi wa afya wanataka kuondoka kabisa Lebanon.

Hali hii inaathiri sekta nyingi, ikiwa ni pamoja na vikosi vya jeshi. Maafisa ambao walikuwa kwenye kozi za mafunzo nchini Ufaransa, Marekani na nchi nyingine wamewasilisha ombi la kujiuzulu na wengine wametoroka na kuamua kusalia katika nchi hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.