Pata taarifa kuu

Takriban watu wakamatwa kuhusiana na kesi ya wanafunzi kupewa sumu

Mamlaka ya Irani inasema imewakamata zaidi ya watu 100 kuhusiana na kisa cha ajabu cha kuwekewa sumu shuleni kwa wasichana.

Watu waliokolewa kutoka shuleni huko Ardabil, baada ya visa vinavyodaiwa kuwa vya sumu, kwenye picha iliyochukuliwa kutoka kwa video ya Machi 1, 2023.
Watu waliokolewa kutoka shuleni huko Ardabil, baada ya visa vinavyodaiwa kuwa vya sumu, kwenye picha iliyochukuliwa kutoka kwa video ya Machi 1, 2023. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Tehran, Siavosh Ghazi

"Zaidi ya watu 100 wanaoshukiwa kuhusika na matukio katika shule wametambuliwa, wamekamatwa na kuhojiwa," Wizara ya Mambo ya Ndani imesema. Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, baadhi ya watu hao walitaka kwa bahati mbaya kufunga shule, huku wengine wakishukiwa kuwa na uhusiano na makundi ya upinzani, hususan Mujahedeen, ambao wanapigana dhidi ya mamlaka ya Iran. Watu hawa walikamatwa katika majimbo kadhaa, yakiwemo yale ya Tehran na Qom kaskazini, mashariki na magharibi mwa Azerbaijan kaskazini magharibi, au yale ya Kurdistan na Hamadan upande wa magharibi.

Maelfu ya wanafunzi walioathirika

Kisa cha kuwekewa sumu wasichana wadogo ambacho kiliathiri shule katika mikoa ishirini kilizua hisia kubwa kote nchini. Tangu mwezi Novemba,kumeshuhudiwa matukio yanayofanana ambapo wasichana wadogo wanaugua kufuatia harufu kali ya gesi. Kwa jumla, mamlaka imeorodhesha zaidi ya wanafunzi 5,000 ambao wameathiriwa katika 'shule 230' katika majimbo 25 ya nchi.

Mapema mwezi Machi, Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alilaani ufalifu huo na kutoa wito wa hukumu kali. Kesi hizi za zilikuja kufuatia maandamano baada ya kifo cha Mahsa Amini aliyekamatwa na polisi wa maadili kwa uvaaji mbaya wa vazi la Kiislamu. Iran ina zaidi ya shule 107,000 na nusu ya wanafunzi milioni 15 wa shule za msingi na sekondari ni wasichana.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.