Pata taarifa kuu

Wanafunzi wapewa sumu nchini Iran: UN yataka kufanyika 'uchunguzi wa uwazi'

Baada ya mfululizo wa visa vya sumu na gesi za ajabu kwa wasichana wadogo tangu mwezi Novemba katika shule za nchini Iran, Umoja wa Mataifa umeungana siku ya Ijumaa na mkuu wa diplomasia ya Ujerumani kuomba ufafanuzi zaidi kuhusiana na visa hivyo.

Watu wakiokolewa shuleni huko Fardis, baada ya kesi zinazodhaniwa za sumu, kwenye picha ya video ya Machi 1, 2023.
Watu wakiokolewa shuleni huko Fardis, baada ya kesi zinazodhaniwa za sumu, kwenye picha ya video ya Machi 1, 2023. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa inahitaji "uchunguzi wa uwazi" na hitimisho la umma. "Tuna wasiwasi na madai haya ambayo wasichana wanalengwa kwa makusudi katika kile kinachoonekana kuwa mazingira ya kushangaza," msemaji wa tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa MataifaRavina Shamdasani amewaambia waandishi wa habari huko Geneva.

Kesi hii ya sumu kwa watu wengi, ambayo imezua sintofahamu na kusababisha minong'ono, ilianza mwishoni mwa mwezi Novemba wakati vyombo vya habari viliripoti kesi za kwanza za sumu kwa njia za kupumua kw mamia ya wasichana wenye umri wa miaka 10 katika shule kadhaa katika Jiji Takatifu la Qom, katikati mwa Iran.

Karibu kesi 800, ikiwa ni pamoja na mia kadhaa siku ya Jumatano 

Jumatano, Machi 1, wanafunzi kutoka shule saba za wasichana katika mji wa Ardabil (Kaskazini) waliripotiwa kupumua vibaya kutiokana na gesi na watu 108 walisafirishwa kwenda hospitalini, mkuu wa huduma za matibabu katika hospitali ya mji huo ameliambia shirika la habari la Tasnim. Hali ya jumla ya wanafunzi, ambao wamepata shida ya kupumua na kupoatwa nakichefuchefu, inaendelea vizuri, amesema. Kesi kadhaa pia ziliripotiwa wiki hii huko Tehran. Katika shule ya upili huko Tehransar, magharibi mwa mji mkuu, wanafunzi waliripotiwa "kupoteza fahamu baada ya kupuliziwa kile kinachodaiwa kuwa gesi au sumu," shirika la habari la Fars, ambalo linanukuu wazazi wa wanafunzi.

Kulingana na makadirio yaliyotolewa Jumatano na msemaji wa Tume ya Afya ya Bunge, Zahra Sheikhi, karibu wanafunzi 800 wameathiriwa tangu kesi za kwanza. Wizara ya Afya ilielezea Jumapili kwamba "watu wengine" walikuwa wakitafuta kwa vitendo hivi "kufunga shule zote, hasa shule za wasichana"

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.