Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Iran: Mfaransa Benjamin Brière aachiliwa huru, lakini (bado) anazuiliwa jela

Jina lake liliitwa kutoka kwa vipaza sauti na wakuu wa gereza. Vifaa vyake vilikuwa vimekusanywa na gari lake lilikuwa linatarajiwa kurejeshwa. Baada ya miaka mitatu akizuiliwa katika gereza la Vakilabad huko Mashhad, mateso ya Mfaransa Benjamin Brière yalikuwa karibu kuisha.

Picha hii isiyo na tarehe iliyopatikana kutoka kwa akaunti ya Twitter ya Saeid Dehghan, wakili wa raia wa Ufaransa Benjamin Brière.
Picha hii isiyo na tarehe iliyopatikana kutoka kwa akaunti ya Twitter ya Saeid Dehghan, wakili wa raia wa Ufaransa Benjamin Brière. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Mtalii huyu mwenye umri wa miaka 37, aliyehukumiwa na mahakama ya mapinduzi mwezi Januari 2022 hadi miaka minane na miezi minane jela kwa "ujasusi" na "propaganda" dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, alikamatwa mwezi Mei 2020 alipokuwa akitumia ndege ndogo isiyo na rubani kwa burudani katika mbuga ya asili kaskazini-mashariki mwa nchi, hukumu yake ilibatilishwa na Mahakama ya Juu, kabla ya kuondolewa mashtaka yote dhidi yake na tawi la 35 la mahakama ya rufaa ya mkoa wa Khorasan Razavi, mnamo Februari 15. Jaji kiongozi wa mahakama hiyo Seyed Hossein Ahmadi Golban ameomba msamaha kwa wakili wake kwa "kosa" ambalo lilihusiana na kkamatwa kwake.

Kuachiliwa kwa Benjamin Brière ilikuwa suala la muda tu. Agizo lilitumwa kwa maafisa wa gereza na hata wakili wake alikuwa ametafutwa ili kumchukua. Hata hivyo, mtalii huyo wa Ufaransa hakuruhusiwa kutoka gereza la Vakilabad. Alama ya jeuri inayotawala katika Jamhuri ya Kiislamu, itabidi arudishwe mahakamani kwa mashtaka yaleyale ya "ujasusi" na "propaganda" dhidi ya Serikali na mahakama hiyo ya rufaa mnamo Juni 12. Kulingana na sheria za Iran, uamuzi wa jaji unapaswa kuwa wa mwisho.

Hatua ya kushangaza

“Hii ni mara ya kwanza kwa mimi binafsi kushuhudia katika mfumo wa mahakama kesi ambapo chumba cha rufaa kinatoa uamuzi na kutoa amri ya kutekelezwa na kuachiwa huru kwa [mteja wangu] na kwamba ninapokea kwa wakati huo huo wito kama vile wakili ukinitaka niripoti tena mbele ya Mahakama ya Rufaa kwa ajili ya mteja wangu Juni 12,” amesema wakili Mahmoud Behzadi Rad katika mahojiano na tovuti ya habari ya Iran ya Emtedadnews. “Hatukukata rufaa hata kidogo! Kesi hiyo ilipelekwa katika Mahakama Kuu ya nchi na ikahamishiwa kwenye mahakama sawa na hiyo, na amri ya kuachiliwa kwa mteja wangu ikatolewa. Ikiwa mpango huu wa kusikitisha unakuwa wa kawaida ndani ya mfumo wa mahakama, basi hakuna chochote cha kutegemea. "

Cha ajabu ni kwamba, mabadiliko haya ya kimahakama yanaonyesha kwa mara nyingine tena mwelekeo wa kisiasa wa jambo hili. Benjamin Brière kwa hakika ni mmoja wa raia saba wa Ufaransa wanaozuiliwa nchini Iran na kuitwa na Ufaransa kama "mateka wa serikali" mikononi mwa Jamhuri ya Kiislamu, ambayo imefanya jambo la ajabu la kuwatia mbaroni raia kutoka nchi za Magharibi katika ardhi yake kwa ajili ya kutekeleza vyema mashinikizo ya kisiasa kwa nchi yao ya asili. Pia, inaonekana kwa mtazamo wa kwanza kwamba Jaji Seyed Hossein Ahmadi Golban, mkuu wa chumba cha thelathini na tano cha mahakama ya rufaa ya mkoa wa Khorasan Razavi, alichukua uamuzi wake wa kumwachilia huru Benjamin Brière "tu" kwa msingi wa sheria, na hivyo "kusahau" suala la kisiasa lililoambatanishwa katika kesi yake mbele ya baadhi ya idara za usalama za Iran. Kubadilika kwake kwa kustaajabisha, siku kumi baada ya kumfutia makosa mtalii huyo wa Ufaransa, unaonyesha kwamba huenda mahakama hiyo ilipata shinikizo.

Mgomo wa njaa

Kiongozi wa kamati ya usaidizi kwa Benjamin Brière, dada yake Blandine Brière hataki kuingia katika masuala haya kwa njia yoyote ile. “Tulipokea hukumu rasmi ya Februari 15 kutoka mahakama ya rufaa ikionyesha kuwa kaka yangu ameachiwa huru na hatuelewi, kwa hiyo, bado anafanya nini gerezani, ameeleza Blandine Brière.

Benjamin aliingia mwezi wake wa pili wa mgomo wa kula mnamo Februari 28, amekumbusha akiwa na wasiwasi. Amepoteza uzito mwingi na anabaki dhaifu. Raia wengine sita wa Ufaransa kwa sasa wanazuiliwa nchini Jamhuri ya Kiislamu. Majina yao ni Fariba Adelkhah, Cécile Kohler, Jacques Paris, Louis Arnaud na Bernard Phelan (raia wa saba wa Ufaransa alikamatwa msimu uliopita wa baridi, lakini jina lake halijajulikana).

Hayo yanajiri wakati mtafiti Mfaransa mwenye asili ya Iran Fariba Adelkhah ambaye alikamatwa mnamo Juni 2019, aliachiliwa kwa mshangao wa kila mtu mnamo Februari 10 kutoka gereza la Evin huko Tehran. hata hivyo, haijulikani katika hatua hii chini ya masharti gani, na ikiwa ataweza kupata pasipoti yake na kuondoka Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.