Pata taarifa kuu

Iran yadai kuzima shambulio la ndege zisizo na rubani kwenye eneo la jeshi Isfahan

Iran imesema imefanikiwa kuzima shambulio la ndege zisizo na rubani kwenye moja ya maeneo yake ya kijeshi katikati mwa mji wa Isfahan.

Picha iliyochukuliwa kutoka kwa video ya UGC iliyotolewa Januari 29, 2023 ambayo inadaiwa kuonyesha mlipuko katika mkoa wa Isfahan nchini Iran.
Picha iliyochukuliwa kutoka kwa video ya UGC iliyotolewa Januari 29, 2023 ambayo inadaiwa kuonyesha mlipuko katika mkoa wa Isfahan nchini Iran. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

 

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Ulinzi, shambulio hilo katika eneo la kijeshi katika mji wa Isfahan lilitekelezwa na vitu vitatu vidogo vya kuruka.

Ndege hizo tatu zisizo na rubani zililipuka zikiwa hewani kabla ya kufikia lengo lao. Moja ilipigwa na mfumo wa ulinzi wa anga na nyingine mbili zililipuka kutokana na mfumo wa kielektroniki wa ulinzi wa anga.

Wizara haikushtumu kundi au nchi yoyote. Lakini huko nyuma, Iran iliituhumu Israel kwa kufanya mashambulizi kadhaa, yakiwemo mashambulizi ya ndege zisizo na rubani, dhidi ya jeshi la nchi hiyo au vituo vya nyuklia.

Mnamo mwezi Aprili 2021, Iran iliishutumu Israeli kwa kushambulia kituo chake cha nyuklia cha Natanz, shambulio ambalo liliharibu karakana ya utengenezaji wa vinu vya kutengeneza uranium iliyorutubishwa. Mnamo 2020, Iran pia ililaumu Israeli kwa shambulio ambalo lilimuua mwanasayansi wake mkuu wa nyuklia.

Eneo la Isfahan lina mitambo mingi ya kijeshi na nyuklia nchini humo. Kwa vyovyote vile, Wizara ya Ulinzi imethibitisha katika taarifa yake rasmi kwamba Iran itaendelea na azma ya mpango wake wa kuimarisha nguvu zake za kijeshi. Hii inaonyesha kuwa eneo lililolengwa lilikuwa muhimu kutoka kwa mtazamo wa kimkakati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.