Pata taarifa kuu

Iran: Tehran yadai kukamilisha kandarasi ya ununuzi wa ndege aina ya Sukhoi Su-35 na Urusi

Iran imetangaza kuwa imekamilisha mkataba na Urusi wa kununua ndege za kivita aina ya Sukhoi Su-35, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti, licha ya Marekani kuonya dhidi ya ushirikiano wa kijeshi kati ya Tehran na Moscow.

Iran imetangaza kwamba imekamilisha kandarasi na Urusi kwa ajili ya ununuzi wa ndege aina ya Sukhoi Su-35 (picha yetu), chombo cha habari rasmi kilisema, licha ya onyo kutoka Marekani.
Iran imetangaza kwamba imekamilisha kandarasi na Urusi kwa ajili ya ununuzi wa ndege aina ya Sukhoi Su-35 (picha yetu), chombo cha habari rasmi kilisema, licha ya onyo kutoka Marekani. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

"Baada ya kuondolewa kwa vikwazo vya [Umoja wa Mataifa] katika ununuzi wa silaha za kawaida mnamo mwezi Oktoba 2020, Iran imekamilisha mkataba wa kununua ndege za kivita za Sukhoi Su-35", limesema shirika la habari la Irna , likinukuu uwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu kwa Umoja wa Mataifa. Shirika hili halikutoa maelezo zaidi kuhusu kandarasi hiyo, lakini Iran na Urusi zimekuwa katika majadiliano kwa miaka mingi kuhusu uwasilishaji wa ndege za kivita za Urusi kwenda Tehran.

'Hatari ya kuzuka kwa vita'

Marekani, adui mkubwa wa Iran, inatishia vikwazo vizito kwa nchi yoyote ile inayofanya biashara na majeshi ya Iran, hususan Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi, jeshi la itikadi kali la Jamhuri ya Kiislamu lililowekwa kwenye orodha yake nyeusi ya "mashirika ya kigaidi". Wakati huo huo, Washington inasikitishwa na kuongezeka kwa "hatari" ya vita kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Iran na Urusi, huku Tehran ikishutumiwa kwa kusambaza ndege zisizo na rubani zinazotumiwa na jeshi la Urusui nchini Ukraine, jambo ambalo Iran inakanusha.

"Sukhoi Su-35s zilikubalika kiufundi na Iran (...) na Urusi ilitangaza kuwa iko tayari kuziuza kwa Jamhuri ya Kiislamu", shirika la habari la Irna limeongeza. Siku ay Jumatatu Waziri wa Ulinzi wa Iran Mohamad-Reza Ashtiani alisema kwamba Tehran "bado inafuatilia ununuzi" wa Sukhoi Su-35, lakini "bado haijapokea vifaa".

Ndege 300 za kivita

Jeshi la Wanahewa la Iran tayari lina ndege 300 za Urusi (Mig-29 na Su-25), ndege kutoka China (F-7), ndehe kutoka Marekani (F-4, F-5 na F-14) na ndege kutoka Ufaransa ( Mirage F1), na vile vile baadhi ya Saeqeh, toleo la Iran la F-5 kutoka Marekani, kulingana na wataalamu. Tehran na Moscow zilitia saini mkataba mwaka 2007 wa kuwasilisha mfumo wa kuzuia makombora wa S-300 wa Urusi, lakini mwaka 2010 Moscow ilisitisha uuzaji huo kwa kutumia azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran.

Mnamo 2015, muda mfupi kabla ya kumalizika kwa makubaliano ya kimataifa juu ya mpango wa nyuklia wa Iran, Moscow iliidhinisha tena uwasilishaji wa mfumo wa kuzuia makombora wa S-300. Mwezi Mei 2016, Wizara ya Ulinzi ya Iran ilisema kwamba nchi hiyo sasa "imemiliki mfumo wa kimkakati wa S-300".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.