Pata taarifa kuu
MAZUNGUMZO-AMANI

Yemen: Mazungumzo juu ya kubadilishana wafungwa yaanza Geneva

Wawakilishi wa serikali na waasi wa Huthi nchini Yemen wameanza mazungumzo juu ya kubadilishana wafungwa huko Geneva Jumamosi, Machi 11, na Umoja wa Mataifa ukitoa wito kwa pande hizo mbili kushiriki katika mazungumzo 'muhimu'.

Wafungwa wa Yemen wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Sanaa kufuatia zoezi la kubadilishana wafungwa, Alhamisi, Oktoba 15, 2020.
Wafungwa wa Yemen wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Sanaa kufuatia zoezi la kubadilishana wafungwa, Alhamisi, Oktoba 15, 2020. AP Photo/Hani Mohammed
Matangazo ya kibiashara

Ufunguzi wa mijadala hii inayotarajiwa kudumu kwa siku 11, unafanyika siku moja baada ya tangazo la kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Saudi Arabia, ambayo inaunga mkono serikali katika vita vyake dhidi ya waasi wa Huthi, na Iran inayounga mkono waasi hao. "Ninatumai kuwa pande zote ziko tayari kushiriki katika mazungumzo muhimu (...) kukubaliana juu ya kuachiliwa kwa wafungwa wengi iwezekanavyo," mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen Hans Grundberg amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

“Wakati (Mwezi wa Mfungo wa Kiislamu) wa Ramadhani unapokaribia, ninazitaka pande husika kuheshimu ahadi walizoweka, sio tu kwa kila mmoja wao, bali hata kwa maelfu ya familia za Yemen ambao wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu  kuungana na familia zao, ” ameongeza. Huu ni mkutano wa saba kutekeleza makubaliano ya kubadilishana wafungwa yaliyofikiwa mjini Stockholm miaka mitano iliyopita, Umoja wa Mataifa umesema.

Kama sehemu ya makubaliano haya, wahusika walikubaliana "kuwaachilia wafungwa wote, wafungwa, watu waliotowejka, watu waliowekwa kizuizini kiholela na wale walio chini ya kizuizi cha nyumbani", katika muktadha wa mzozo ambao umedumu tangu mwaka 2014 chini Yemen, "bila ubaguzi au sharti lolote". Mikutano ambayo imefanyika huko nyuma, iliyopatanishwa na Umoja wa Mataifa, tayari "imesababisha kuachiliwa kwa wafungwa wa pande zote mbili", Shirikisho la Vyama vya Msalaba Mwekundu, ICRC, limeliambia shirika la habari la AFP.

'Kufikia makubaliano juu ya maelezo ya kubadulihana wafungwa'

Mnamo mxaka 2020, kwa mfano, "zaidi ya wafungwa 1,050 waliachiliwa na kurudishwa katika eneo lao la asili au nchi yao ya asili", kulingana na chanzo hicho. "ICRC imejitolea kusaidia utekelezaji wa kuachiliwa kwa wafungwa kwa siku zijazo na kubadilishana kwa wafungwa, na kuwarudisha au kuwahamisha wafungwa walioachiliwa kutoka mstari wa mbele hadi kwa nyumba zao," shirika hilo limesema.

Lengo la mazungumzo hayo ni "kufikia makubaliano juu ya maelezo" ya kubadilishana wafungwa, amesema Majed Fadail, mjumbe wa ujumbe wa serikali ya Yemen, aliyenukuliwa na shirika la habari la serikali la Saba. Katika ujumbe uliotumwa kwenye Twitter, mjumbe mkuu wa Hothi kwenye mazungumzo ya Geneva, Abdelkader Al-Mourtada, amesema anatumai kuwa duru hii ya mazungumzo itakuwa 'ya maamuzi'.

Mwishoni mwa mwezi Machi 2022, waasi  wa Huthi walitangaza kubadilishana wafungwa hali ambao iliwezesha waasi 1,400 na wapiganaji 823 kutoka kwa vikosi vinavyounga mkono serikali kurejea kwenye kambi zao. Tangazo hili lilifuatiwa na mikutano huko Amman, lakini bila maendeleo madhubuti.

Waasi wa Hothi walichukua udhibiti wa mji mkuu wa Yemen Sanaa mapema mwaka 2015, na kusababisha uingiliaji kati mwezi Machi mwaka huo  wa muungano unaoongozwa na Saudi Arabia kuunga mkono serikali. Tangu wakati huo, vita hivyo vimegharimu mamia ya maelfu ya maisha ya watu na kuitumbukiza nchi hii, maskini zaidi kwenye Rasi ya Arabia, katika moja ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu duniani.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.