Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

Iran yamnyonga naibu Waziri wake wa ulinzi wa zamani Alireza Akbari

Raia wa Uingereza na Iran Alireza Akbari, aliyekuwa amepewa adhabu ya kifo nchini Iran, amenyongwa, baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na ujasusi kwa ajili ya nchi ya Uingereza.

Alireza Akbari alipatikana na hatia ya ya kujihusisha na ujasusi kwa ajili ya nchi ya Uingereza.
Alireza Akbari alipatikana na hatia ya ya kujihusisha na ujasusi kwa ajili ya nchi ya Uingereza. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kunyongwa kwa naibu Waziri huyo wa ulinzi wa zamani wa Iran, kunakuja baada ya kukamatwa mwaka 2019 na kufunguliwa mashtaka ya ujasusi kwa manufaa ya nchi ya Uingereza. 

Ripoti zinasema, família ya Akbari, iliombwa kwenda katika gereza alilokuwa anazuiwa, ili kumtazama ndugu yao na kumwona kwa mara ya mwisho, wiki hii. 

Iran ilidai kuwa, Akbari alipewa adhabu hiyo kwa sababu ya kutishia na kuharibu usalama wake wa ndani na nje kwa kutoa taarifa za kiinteljensia kwa taifa la kigeni. 

Serikali ya Uingereza, ikiongozwa na Waziri Mkuu Rishi Sunak, imelaani kitendo hicho na kusema, ni kitendo cha kinyama, kinachoonesha udhaifu wa serikali ya Tehran. 

Marekani nayo, hapo awali, ilikuwa imeitaka Iran kutotekeleza adhabu hiyo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.