Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Mahakama yatoa hukumu mpya dhidi ya waandamanaji waliokamatwa

Baada ya vijana wawili kunyongwa, Jumamosi Januari 7, kwa madai ya mauaji ya mwanamgambo wa Kiislamu mnamo Novemba 3, 2022, nchi nyingi zimeelezea kutiwa wasiwasi juu ya utumiaji wa hukumu mpya za kifo na mahakama nchini Irani.

Wanawake na wanaume wamekuwa wakiandamana kwa wiki kadhaa kuupinga utawala wa Kibepari na ukatili wake katika mitaa ya Tehran na kote nchini.
Wanawake na wanaume wamekuwa wakiandamana kwa wiki kadhaa kuupinga utawala wa Kibepari na ukatili wake katika mitaa ya Tehran na kote nchini. AP
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zilisambazwa Jumapili, Januari 8, kuhusu uwezekano wa kutumika kwa hukumu ya kifo dhidi ya vijana wawili, Mohammad Ghebadlou na Mohammad Boroughani. Wa kwanza alishtakiwa kwa kuendesha gari lake kwenye kundi la maafisa wa polisi na kumuua mmoja wao. Wazazi wa Mohammad Ghebadlou na watu kadhaa walikusanyika usiku kucha mbele ya gereza la Rejai-Shahr kutaka hukumu ya kifo isitumike.

Adhabu ya kifo imethibitishwa

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran, Mahakama ya Juu imeidhinisha hukumu ya kifo dhidi ya takriban watu 15 waliokamatwa katika miezi ya hivi karibuni kwa hatua dhidi ya usalama wa taifa na mashambulizi ya silaha. Asubuhi ya leo, shirika la habari la Tasnim limetangaza kuwa hukumu tatu mpya za kifo zimetolewa huko Isfahan kwa mauaji ya maafisa watatu wa vikosi vya usalama.

Nia ya serikali

Tangu kuanza kwa maandamano, watu wanne wamenyongwa na makumi ya wengine wamehukumiwa vifungo vikali kwa kuhatarisha usalama wa umma. Mamlaka inaonekana kudhamiria kuchukua hatua kwa uamuzi licha ya jamii ya kimataifa kulaani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.