Pata taarifa kuu

Ufaransa: Muiran ajiua kutokana na hali inayoendelea nchini mwake

"Unapotazama video hii, nitakuwa nimefariki": ni maneneo ya raia mmoja wa Iran aliyejiua Jumatatu, Desemba 26, kwa kujitupa kwenye Mto Rhône huko Lyon, anasema kwenye video baada ya kifo chake, kutokana na hali ya nchi yake. , inayokabiliwa na maandamano.

Mnamo Desemba 27, heshima za mwisho zilitolewa huko Lyon kwa Muiran huyu aliyejiua kwa kujitupa kwenye Mto Rhône kukemea ukandamizaji nchini Iran.
Mnamo Desemba 27, heshima za mwisho zilitolewa huko Lyon kwa Muiran huyu aliyejiua kwa kujitupa kwenye Mto Rhône kukemea ukandamizaji nchini Iran. AFP - JEFF PACHOUD
Matangazo ya kibiashara

 

Raia huyu wa Iran alipatikana amekufa maji Jumatatu alasiri, polisi imeliambia shirika la habari la AFP, na kuthibitisha habari kutoka kwa gazeti la Le Progrès. Mtu huyo, mwenye umri wa miaka 38 kwa mujibu wa video yake.

Iran inakumbwa kwa muda wa miezi mitatu na wimbi la maandamano ambayo hayajawahi kutokea tangu Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979. Maandamano hayo yalianza na madai ya haki za wanawake baada ya kifo cha Mahsa Amini, katikati ya mwezi wa Septemba, aliyekamatwa kwa kuvaa vazi la Kiislamu kimakosa. Maandamano ya kudai uhuru wa wanawake taratibu yalibadilika na kuwa harakati pana zaidi iliyoelekezwa dhidi ya utawala wa Kiislamu. Wakuu, ambao wanashutumu "machafuko", walikamata maelfu ya watu na kuwahukumu kumi na wawili wao kifo kwa kuhusika kwao katika harakati hizi za maandamano.

"Polisi wanashambulia watu, tumepoteza watoto wengi wa kiume na wa kike, lazima tufanye kinachohitajika", anasema mwanaume huyo kwa sauti ya utulivu kwenye video hii iliyowekwa kwenye mitandao kadhaa ya kijamii kabla ya kujiua.

Waunge mkono watu wa Iran katika vita vyao 'dhidi ya serikali yenye vurugu'

"Nimeamua kujitoa uhai katika mto Rhone, ni changamoto kuonyesha kwamba sisi, raia wa Iran, tumechoka na hali hii" alibaini. "Unapotazama video hii, nitakuwa nimekufa", ameongeza, kabla ya kutoa wito wa kuungwa mkono kwa raia wa Iran katika vita vyao dhidi ya "polisi na serikali yenye vurugu kubwa".

Wito wa mkutano wa hadhara, Jumanne, Desemba 27 baada ya alasiri katikati mwa jiji la Lyon, ili kumuenzi, umezinduliwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mwanzoni mwa mwezi wa Desemba, viongozi wa Iran walijaribu kuwatuliza nyoyo waandamanaji, kwa kutangaza kufutwa kwa polisi ya maadili. Lakini katika mchakato huo, mamlaka iliwaua kwa kuwanyonga vijana wawili, waliotiwa hatiani kwa vitendo vinavyohusiana na maandamano hayo.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.