Pata taarifa kuu

Iran: Muandamanaji mwingine anyongwa hadharani

Kijana mwenye umri wa miaka 23 amenyongwa nchini Iran Jumatatu, Desemba 12, kulingana na serikali kwa mauaji ya wanamgambo wawili wa Kiislamu, siku nne baada ya kunyongwa kwa Mohsen Shekari ambaye alishtakiwa kwa kumchoma kisu mmoja wa wanamgambo wa Kiislamu wakati wa maandamano ambayo yametikisa nchi kwa miezi mitatu sasa.

Bango dhidi ya adhabu ya kifo wakati wa maandamano dhidi ya utawala wa Iran yaliyoandaliwa mjini Berlin, Desemba 10, 2022.
Bango dhidi ya adhabu ya kifo wakati wa maandamano dhidi ya utawala wa Iran yaliyoandaliwa mjini Berlin, Desemba 10, 2022. REUTERS - MICHELE TANTUSSI
Matangazo ya kibiashara

Kunyongwa kwa Majid Reza Rahnavard kulifanyika hadharani Jumatatu asubuhi katika mji mtakatifu wa Macchad, anaandika mwandishi wetu huko Tehran, Siavosh Ghazi. Kijana huyu mwenye umri wa miaka 23 alikamatwa mnamo Novemba 19 kwa mauaji ya wanamgambo wawili wa Kiislamu, maarufu bassidjis, siku mbili kabla, kwa mujibu wa Tehran. Takriban siku ishirini zilipita, kati ya kukamatwa kwake na kuuawa kwake.

Tangu kifo cha Mahsa Amini, Septemba 16, Mkurdi wa Iran mwenye umri wa miaka 22, aliyefariki baada ya kukamatwa na polisi inayoheshilisha maadili kwakukiuka sheria ya mavazi ya Jamhuri ya Kiislamu, Iran imeendelea ikikumbwa na maandamano.

Kesi iliyoharakishwa

Mamlaka imerusha video mbili zilizonaswa na kamera za CCTV. Kwenye video hizi, anaonekana mtu mmoja mwanamume, aliyewasilishwa kwa jina la Majid Reza Rahnavard, akimshambulia kijana mmoja katikati ya barabara na kumdunga kisu mara kadhaa. Kisha, mshambuliaji anageuka na kumchoma kisu kijana mwingine ambaye amekuja kusaidia. Bassidji hao wawili walikufa papo hapo. Katika kutoroka kwake, mshambuliaji pia aliwajeruhi wapita njia wanne, kulingana na mamlaka.

Amehukumiwa kwa kosa la moharebeh au "vita dhidi ya Mungu na ufisadi duniani", kosa ambalo lilimfanya ahukumiwe kifo. Mashirika ya haki za binadamu yanashutumu kesi ya haraka na ukweli kwamba Majid Reza Rahnavard hakuweza kuchagua wakili wake mwenyewe.

Fanny Gallois, mkuu wa mpango wa Uhuru katika Amnesty International, anatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kuepuka kunyongwa kwa watu wengine.

Ni muhimu kwamba jumuiya ya kimataifa isikae kimya kwa sababu umwagaji damu unatarajiwa, si tena mitaani, bali katika mahakama.

Kwa upande wake, "Ufaransa inalaani vikali kunyongwa hadharani leo kwa mwanamume wa Iran aliyehukumiwa kifo kufuatia kushiriki kwake katika maandamano", imetangaza Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa, ikilaani tena " ukiukwaji mkubwa na usiokubalika wa haki za kimsingi na uhuru unaofanywa na mamlaka ya Iran”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.