Iran: Watu watano wahukumiwa kifo kwa mauaji ya mwanamgambo wa Kiislamu
Mahakama ya Iran imetangaza hukumu mpya za kifo dhidi ya watu watano huku kukiwa na miito ya mgomo wa siku tatu na maandamano kuanzia Jumatatu tarehe 5 hadi siku ya Jumatano.
Imechapishwa:
Jumla ya watu kumi na watano wamehukumiwa kwa mauaji ya mwanamgambo wa Kiislamu au bassidji wiki chache zilizopita. Watu watano walihukumiwa kifo na wengine hukumu nzito.
Video ya mauaji hayo ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya serikali na ilitumika katika kesi hiyo. Katika video hiyo kunaonekana watu wapatao thelathini wakimshambulia kijana kwa kisu na mawe, pia wakimpiga teke.
Hukumu mpya za kifo zilitangazwa huku waandamanaji wanne au wasumbufu, kulingana na mamlaka, walinyongwa Jumapili asubuhi.
Kadhalika, mkuu wa mahakama alitangaza kunyongwa katika siku zijazo kwa watu waliopatikana na hatia ya mauaji wakati wa maandamano ya wiki chache zilizopita.
Jumanne hii, kulikuwa na maduka machache yaliyofungwa katika mji mkuu kuliko Jumatatu. Jana usiku, makundi madogo ya vijana walifanya maandamano katika vitongoji kadhaa vya Tehran, huku wakizuia njia na barabara kuu katika mji mkuu.
Wakati huo huo, msemaji wa vyombo vya sheria ametangaza kwamba waandamanaji 1,200 waliokamatwa katika wiki za hivi karibuni wameachiliwa.