Pata taarifa kuu
IRAN - USALAMA

Iran imekivunja Kikosi maalumu cha polisi wa maadili baada ya maandamano

Mamlaka nchini Iran, zimetangaza kukivunja kikosi maalumu cha polisi ya maadili, hatua inayokuja baada ya karibu miezi miwili ya maandamano ya raia, waliokuwa wakipinga mauaji yua msichana Mahsa Amini aliyeuawa akiwa mikononi mwa polisi hao.

Waandamanaji wakichoma moto magurudumu ya magari nchini Iran
Waandamanaji wakichoma moto magurudumu ya magari nchini Iran © Réseaux sociaux
Matangazo ya kibiashara

Maandamano ya raia dhidi ya polisi hao, yalianza siku chache baada ya taarifa za kuuawa kwa msichana Mahsa Amini, ambaye alikamatwa kwa madai ya kukiuka sheria za mavazi ya wanawake.

Tangu wakati huo, maelfu ya wanawake nchini humo wamekuwa wakijotokeza barabarani, kukashifu polisi hao, huku wakichoma moto hijabu zao na kuimba nyimbo za kuukashifu utawala wa Tehrani.

Kwa mujibu wa mwanasheria mkuu wa Serikali ya Iran, Mohammad Jafar Montazeri, amesema serikali imesikia kilio cha wananchi na kwamba wanakivunja rasmi kikosi hicho alichosema hakina mamlaka kisheria.

Uamuzi huu umepokelewa kwa hisia mseto na mashirika ya kutetea haki za binadamu yanayotaka polisi waliohusika na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu, kuadhibiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.