Pata taarifa kuu
HAKI-MAANDAMANO

Iran: Siku tatu za mgomo kuanzia Jumatatu hii, serikali yatangaza kunyongwa ka watu kadhaa

Nchini Iran, wito umetolewa kwa siku tatu za mgomo na maandamano dhidi ya mamlaka kuanzia Jumatatu hii, Desemba 5, wakati Waziri wa Sheria amepotangaza kunyongwa tena kwa waandamanaji wanaotajwa kama 'wasumbufu'.

Iran: Wito wa maaandamano na mgomo umeitikiwa huko Sanandaj, Kurdistan ya Iran, Jumatatu hii, Desemba 5, 2022.
Iran: Wito wa maaandamano na mgomo umeitikiwa huko Sanandaj, Kurdistan ya Iran, Jumatatu hii, Desemba 5, 2022. AFP - BASMA BADRAN
Matangazo ya kibiashara

Huko Tehran, idadi ya maduka ambayo haijabainishwa lakini kubwa imefungwa Jumatatu, Desemba 5. Kulingana na video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hali inaripotiwa kufanana katika miji kadhaa ya mkoa huo, hasa katika miji ya Shiraz na Isfahan. Katika miji ya Kurdistan ya Iran, maandamano na mgomo vinaonekana kuitikiwa zaidi.

Mkuu wa idara ya mahakama amesema Jumatatu kuwa wale waliotishia wafanyabiashara na wasafirishaji wa malori kuwalazimisha kuacha kazi watatambuliwa na kuadhibiwa. Serikali pia imefunga moja kwa moja baadhi ya maduka ambayo yalikuwa yamefungwa, ikiwa ni pamoja na mgahawa na duka la vito la mwanasoka wa zamani wa kimataifa Ali Daie, ambaye alitangaza kufungwa kwa maduka yake ili kuunga mkono maandamano.

Katika muktadha huu, mkuu wa idara ya sheria alitangaza kwamba hukumu ya kifo dhidi ya ya baadhi ya wasumbufu wanaohusishwa na idara za ujasusi za kigeni, hasa Israeli - hasa wale waliofanya mauaji kwa silaha - imethibitishwa na itatekelezwa hivi karibuni.

Tayari watu wanne wamenyongwa siku ya Jumapili kwa sababu hizo. Watu hao ambao walitajwa kama "majambazi", waliuawa kwa kunyongwa kwa madai ya uharibifu wa mali ya umma na utekaji nyara. Kulingana na vyombo vya habari vya Iran, watu hawa wanne pia walipatikana na hatia ya uhusiano na idara ya kijasusi ya Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.