Pata taarifa kuu

Iran yavunja polisi inayoheshimisha maadili

Ni polisi inaoheshimisha maadili iliyomkamata Mahsa Amini mwezi Septemba, ikimtuhumu kutoheshimu kanuni za mavazi. Kifo chake kilitangazwa siku tatu baadaye.

Maandamano mjini Tehran, Septemba 19, 2022.
Maandamano mjini Tehran, Septemba 19, 2022. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Iran imetangaza kuvunja polisi inayoheshimisha maadili iliyohusika na kukamatwa kwa Mahsa Amini, ambaye kifo chake akiwa kizuizini kimeibua wimbi la maandamano nchini Iran ambayo yamedumu kwa takriban miezi mitatu.

Tangazo hilo, ambalo linaonekana kama ishara kwa waandamanaji, limekuja baada ya mamlaka kuamua Jumamosi kurekebisha sheria ya 1983 juu ya usiri wa lazima nchini Iran, iliyowekwa miaka minne baada ya mapinduzi ya Kiislamu ya 1979.

Ni polisi inayoheshimisha maadili iliyomkamata Mahsa Amini, Mkurdi wa Iran mwenye umri wa miaka 22, mjini Tehran mnamo Septemba 13, ikimtuhumu kutoheshimu sheria kali ya mavazi katika Jamhuri ya Kiislamu, inayowataka wanawake kuvaa hijabu mbele ya hadhira.

Kifo chake kilitangazwa siku tatu baadaye. Wanaharakati na familia yake wanasema Mahsa Amini alifariki baada ya kupigwa, lakini mamlaka imehusisha kifo chake na masuala ya afya, jambo ambalo wazazi wake wamekanusha.

Kifo chake kilizusha wimbi la maandamano ambapo wanawake, walioanzisha maandamano hayo, walivua na kuchoma hijabu zao, wakipiga kelele "Mwanamke, maisha, uhuru".

Licha ya ukandamizaji uliosababisha vifo vya mamia, maandamano yanaendelea.

"Polisi inayoheshimisha maadili (...) imefutwa na wale walioiunda," Mwanasheria Mkuu Mohammad Jafar Montazeri amesema Jumamosi jioni, akinukuliwa na shirika la habari la Isna siku ya Jumapili.

Kikosi hiki cha polisi, kinachojulikana kama Gasht-e Ershad (doria elekezi), kiliundwa chini ya Rais wa kihafidhina Mahmoud Ahmadinejad, "kueneza utamaduni wa adabu na hijabu". Inaundwa na wanaume waliovaa sare za kijani na wanawake waliovaa chador nyeusi, ambayo hufunika kichwa na sehemu ya juu ya mwili.

Kitengo hiki kilianza doria zake za kwanza mnamo 2006.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.