Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Iran yamnyonga mtu aliyehusika katika maandamano

Mtu huyo aliyepata adhabu hiyo, amebainika kwa jina la Mohsen Shekari baada ya kukamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa kosa la kumshambulia afisa wa usalama kwa kutumia kisu wakatu wa maandamano jijini Tehran. 

Mwanamke huyu akiwa katika moja ya maeneo ya mji mkuu wa Iran, Tehran, Oktoba 11, 2022.
Mwanamke huyu akiwa katika moja ya maeneo ya mji mkuu wa Iran, Tehran, Oktoba 11, 2022. AFP - ATTA KENARE
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya uongozi nchini humo kusema itaendelea kuwachukulia hatua kali, wale wote wanaoshiriki kwenye maandamano yanayoendelea. 

Manadamano nchini Iran, yamekuwa yakiendelea tangu mwezi Septemba, baada ya kuuawa kwa mwanamke mwenye umri wa miaka 22 Mahsa Amini, ambaye alikamatwa na baadaye kuuawa baada ya kudaiwa, kutovaa kwa kuheshimu kanuni za nchi hiyo. 

Awali, Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la  Amnesty International lilikuwa limeonya kuwa, matukio ya waandamanaji waliokamatwa kupewa adhabu ya kifo yangetekelezwa. 

Serikali ya Ufaransa imelaani kuuawa kwa mwaandamanaji huyo, na kusema kilichotokea, hakikubaliki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.