Pata taarifa kuu

Iran: EU 'yasikitishwa' na hukumu ya kifo dhidi ya watu wawili kuhusiana na maandamano

Umoja wa Ulaya umesema "unashangazwa" na kunyongwa nchini Iran kwa Mohammad Mehdi Karami na Seyyed Mohammad Hosseini, waliokamatwa na kuhukumiwa kifo kuhusiana na maandamano yanayoendelea nchini humo, amesema msemaji wa Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell.

Maandamano mjini Tehran, mji mkuu wa Iran, tarehe 1 Oktoba 2022.
Maandamano mjini Tehran, mji mkuu wa Iran, tarehe 1 Oktoba 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

 

Umoja wa Ulaya, ambao unashutumu "ishara mpya ya ukandamizaji wa maandamano", "kwa mara nyingine tena inatoa wito kwa mamlaka ya Iran kukomesha mara moja tabia inayolaumiwa ya kutamka na kutekeleza hukumu za kifo dhidi ya waandamanaji" na "kufuta haraka 'hukumu za kifo za hivi majuzi ambazo tayari zimetolewa katika muktadha wa maandamano,” Nabila Massrali ameongeza katika taarifa yake.

Wanaume wawili walinyongwa Jumamosi, Januari 7, nchini Iran baada ya kupatikana na hatia na mahakama ya Iran ya kumuua mwanajeshi wakati wa maandamano yaliyosababishwa na kifo cha kijana mmoja Mkurdi aliyepatikana amefariki dunia akiwa gerezani, shirika la habari la vyombo vya sheria Mizan Online, limetangaza.

Vijana wawili walionyongwa Jumamosi hii asubuhi ni Mohammad Mehdi Karami na Mohammad Hosseini. Walishtakiwa pamoja na watu wengine kumi na wanne kwa mauaji ya mwanamgambo wa Kiislamu mapema mwezi Novemba wakati wa maandamano ya kupinga mamlaka. Kulikuwa na uhamasishaji mkubwa wa kimataifa hasa wa kumuunga mkono Mehdi Karami uliowasilishwa na wazazi wake kama bingwa wa karate.

Video

Video zilizochukuliwa na waandamanaji zilionyeshwa wakati wa kesi hiyo zikiwaonyesha takriban watu 30 wakimshambulia mwanamgambo wa Kiislamu Rouhollah Ajamian kwa mawe au visu. Mahakama ilikuwa imewahukumu kifo watu watano katika kesi hii lakini Mahakama ya Juu ilifutilia mbali hukumu za watu wengine watatu. Katika siku za hivi karibuni, vyombo vya habari vya serikali vilitangaza kwamba hukumu ya kifo ya takriban watu kumi na tano waliokamatwa katika miezi ya hivi karibuni ilithibitishwa na Mahakama ya Juu.

Waandishi wa habari wakamatwa

Hukumu ya kifo ilitekelezwa kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa mwezi wa Desemba. Mohsen Shekari alinyongwa mnamo Desemba 8 kwa kumshambulia mwanamgambo wa Kiislamu kwa kisu. Kijana mwingine, Majidreza Rahnavard, alinyongwa hadharani tarehe 12 Desemba. Alipatikana na hatia na mahakama ya Iran kwa kuwaua wanamgambo wawili wa Kiislamu katika mji wa Mashhad. Mamlaka pia ilitangaza kukamatwa kwa watu wengine katika siku za hivi karibuni, wakiwemo waandishi wa habari wanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.