Pata taarifa kuu
SIASA-HAKI

Israel: Malengo ya serikali mpya ya Benjamin Netanyahu kabla ya kula kiapo

Serikali ya Israeli itawasilishwa kwa Bunge (Knesset) Alhamisi hii, Desemba 29 , ambalo litpiga kura ya imani katika muungano huu mpya uliopingwa na upinzani. Lakini ugawaji wa nyadhifa za mawaziri utaendelea hadi dakika ya mwisho.

Benyamin Netanyahu atatangaza serikali yake mpya, yenye msimamo mkali.
Benyamin Netanyahu atatangaza serikali yake mpya, yenye msimamo mkali. Gali Tibbon/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Takriban miezi miwili baada ya uchaguzi, hatimaye ni asubuhi ya Alhamisi hii, Desemba 29 ambapo Benyamin Netanyahu atatagaza serikali yake mpya. Hii ni serikali ya sita atakuwa ameongoza.

Mpango wa kisiasa wa muungano wa serikali ulichapishwa ndani ya saa 24 kabla ya kuapishwa, kama inavyotakiwa na sheria. Inajumuisha kuanza tena kwa ujenzi katika makazi katika Ukingo wa Magharibi, kurejesha hukumu ya kifo kwa wahusika wa mashambulizi ya kigaidi, mapambano dhidi ya uhalifu katika maeneo ya Waarabu, bei ya chini na usafiri bora wa umma.

Waziri wa zamani aliyekuwa mpenzi wa jinsia moja kuongoza Bunge (Knesset)

Kijadi, malengo machache sana ya programu za kisiasa yamefikiwa. Lakini msisitizo maalum wakati huu umewekwa kwenye mageuzi ambayo yatazuia Mahakama ya Juu dhidi ya kupinga sheria.

Ugawaji wa nyadhifa za mawaziri unaendelea hadi dakika ya mwisho. Na ili kuondoa hofu ya jamii ya wapinzi wa jinsia moja (LGBT+), waziri mkuu ametoa wadhifa wa spika wa Bunge (Knesset) kwa waziri wa zamani Amir Ohana, ambaye mwenyewe ni mpenzi wa jinsia moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.