Pata taarifa kuu
SIASA-USALAMA

Israel: Netanyahu apata siku 10 kuunda serikali

Ijumaa hii, Desemba 9, Rais wa Israel Isaac Herzog ametangaza kwamba amempa Waziri Mkuu mteule Benyamin Netanyahu siku kumi za ziada kuunda serikali yake pamoja na washirika wake kutoka vyama vya mrengo wa kulia na vya kidini.

Akiwa ameshinda uchaguzi wa wabunge mnamo Novemba 1 na washirika wake wa siasa kali za mrengo wa kulia na Waorthodox, Benjamin Netanyahu (picha yetu) aliteuliwa mnamo Novemba 13 kuunda serikali mpya.
Akiwa ameshinda uchaguzi wa wabunge mnamo Novemba 1 na washirika wake wa siasa kali za mrengo wa kulia na Waorthodox, Benjamin Netanyahu (picha yetu) aliteuliwa mnamo Novemba 13 kuunda serikali mpya. © Ariel Schalit/AP
Matangazo ya kibiashara

Siku ay Alhamisi hii jioni, Desemba 8, chini ya siku tatu kabla ya tarehe ya mwisho ya Desemba 11 kuunda serikali, Bw. Netanyahu alimwomba Rais Herzog aongezewe muda wa wiki mbili, jambo ambalo kwa kiasi fulani lilikubaliwa. “Ninakupa muda wa siku kumi, yaani hadi Jumatano, Desemba 21, kuwasilisha serikali,” Bw. Herzog amemuandikia Waziri Mkuu mteule, katika barua iliyochapishwa na ofisi yake.

'Tuko katikati ya mazungumzo'

Baada ya kushinda uchaguzi wa wabunge wa Novemba 1 na washirika wake wa mrengo mkali wa kulia na wa Orthodox, Benyamin Netanyahu aliteuliwa mnamo Novemba 13 kuunda serikali ndani ya siku 28 baada ya uteuzi huo, pamoja na uwezekano wa kuomba muda wa ziada wa siku 14. "Tuko katikati ya mazungumzo na tumepata maendeleo mengi, lakini kwa kuangalia kasi ya mambo, nitahitaji siku zote za kuongeza muda zilizotolewa na sheria ili kuunda serikali," Netanyahu alimuandika rais wa Israel siku ya Alhamisi.

Katika majibu yake, Ijumaa hii, Desemba 9, Isaac Herzog, ambaye tayari alikuwa ameonyesha hofu kuhusu baadhi ya washirika wa muungano wa Bw. Netanyahu, anamuomba kuunda serikali 'kwa maslahi ya taifa la Israel na wananchi wake' na kuheshimu watu kutoka jamii mbalimbali.

Katika mazungumzo hayo, Likud ya Binjamin Netanyahu tayari imetoa nyadhifa nyeti kwa watu wenye utata kama vile kiongozi wa mrengo wa kulia Itamar Ben Gvir, anayepinga Wapalestina, na Avi Maoz, anayejulikana kwa misimamo yake dhidi ya wapenzi wa jinsi moja, LGBTQ.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.