Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Israel: Benjamin Netanyahu kurejea tena mamlakani

Muungano wa siasa wa mrengo wa kulia wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, umeshinda idadi kubwa ya viti bungeni, hatua inayomruhusu kurejea tena madarakani. 

Wafuasi wa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa zamani wa Israel na mkuu wa chama cha Likud wakisherehekea matokeo ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge, katika makao makuu ya chama cha Likud mjini Jerusalem, Jumatano, Novemba 2, 2022.
Wafuasi wa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa zamani wa Israel na mkuu wa chama cha Likud wakisherehekea matokeo ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge, katika makao makuu ya chama cha Likud mjini Jerusalem, Jumatano, Novemba 2, 2022. AP - Tsafrir Abayov
Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo wa wabunge, yanaonesha kuwa, muungano wa Netanyahu, umeshinda viti 64 kati ya viti 120 vilivyokuwa vinawaniwa. 

Chama cha Netanyahu cha Likud, katika muungano huo, umefanikiwa kupata viti 32. 

Netanyahu, amewaambia wafuasi wake kuwa ataunda, serikali thabiti ya kitaifa. 

Wapinzani wa Netanyahu, muungano unaongozwa na Waziri Mkuu wa sasa, Yair Lapid, kimefanikiwa kupata viti 51 na tayari, kiongozi huyo wa sasa amekubali kushindwa na kuagiza ofisi yake kuanza mchakato wa makabidhiano ya madaraka. 

Netanyahu ambaye amepata ushindi, katika kipindi ambacho amefuguliwa mashtaka ya ufisadi, anatarajiwa kuagizwa na rais Isaac Herzog kuunda serikali, kuanzia wiki ijayo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.