Pata taarifa kuu

Israel: Benjamin Netanyahu apewa jukumu la kuunda serikali mpya

Kufuatia uchaguzi wa wabunge wa Novemba 1, Benjamin Netanyahu ametakiwa na rais wa Israel kuunda serikali mpya. Ana siku 42 kukamilisha kazi hii.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa zamani wa Israel na kiongozi wa chama cha Likud, akiwasalimia wafuasi wake, Jumatano, Novemba 2, 2022.
Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa zamani wa Israel na kiongozi wa chama cha Likud, akiwasalimia wafuasi wake, Jumatano, Novemba 2, 2022. © AP/Maya Alleruzzo
Matangazo ya kibiashara

“Nitakuwa Waziri Mkuu wa wote, wa wale waliotupigia kura, lakini pia wa wengine wote. Ni jukumu langu,” amesema Binyamin Netanyahu alipokuwa akianzisha uundwaji wa serikali mpya ya Israel.

Akifaulu kuunda serikali mpya, itakuwa ni mara ya sita kwa kiongozi huyo anayeitwa pia “Bibi” kuwa Waziri Mkuu. Kwa upande mwingine, wakati huu atakuwa mkuu wa serikali ya mrengo wa kulia zaidi katika historia ya nchi hii.

Kinadharia, kazi hiyo haionekani kuwa gumu kwani wabunge 64 waliochaguliwa kati ya 120 walimpa uungwaji mkono wa kuunda muungano huo. Hivyo, Waziri Mkuu mteule amefikiri angeweza kutangaza serikali yake Jumatano hii. Lakini kiutendaji, mambo yanaonekana kuwa rahisi sana kwa sababu ya hamu kubwa ya washiriki watano wa Likud, chama cha Netanyahu.

Kugawana nyadhifa za mawaziri itakuwa jamo gumu kufanikiwa. Wizara ya Usalama wa Taifa na Wizara ya Ulinzi znaweza kupewa hasa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha ubaguzi wa rangi na ushoga.

Mpango wa kisiasa pia unajadiliwa. Unatetea uimarishwaji wa makazi, mashambulizi kwa Mahakama ya Juu na kutotambuliwa kwa waongofu kwa Uyahudi unaofanywa na marabi wasiokuwa Waorthodoksi.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu ameahidi "serikali imara na yenye ufanisi, serikali inayowajibika na yenye kujitolea".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.