Pata taarifa kuu

Waziri Mkuu mpya wa Israel ameahidi kuliunganisha taifa hilo lililoshuhudia mpasuko

Waziri Mkuu mpya wa Israli Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo ambalo limeshuhudia uchaguzi mara nne ndani ya kipindi cha miaka miwili. Ametoa kauli hii baada ya wabunge kupitisha kuunda kwa serikali ya muungano kwa kupata ushindi mwembamba wa kura 60 kwa 59. 

Jerusalem: kupeana mikono baridi kati ya washirika wawili wa zamani ambao wamekuwa wapinzani: Benjamin Netanyahu (L) anasalimiana na mrithi wake kama Waziri Mkuu, Naftali Bennett (L), mnamo Juni 13, 2021 huko Knesset.
Jerusalem: kupeana mikono baridi kati ya washirika wawili wa zamani ambao wamekuwa wapinzani: Benjamin Netanyahu (L) anasalimiana na mrithi wake kama Waziri Mkuu, Naftali Bennett (L), mnamo Juni 13, 2021 huko Knesset. AP - Ariel Schalit
Matangazo ya kibiashara

Knesset, Bunge la Israeli lilithibitisha serikali mpya ya Naftali Bennett Jumapili jioni. Waziri mkuu huyo mpya alikuwa na wakati mgumu kutoa hotuba yake. Katika bunge la Knesset, kuna wimbi la unyanyasaji. Anaitwa mwongo, mkorofi, kwanza na washiriki wa vuguvugu la Wazayuni wa kidini, halafu na viongozi waliochaguliwa wa Likud, chama cha Benjamin Netanyahu.

Naftali Bennett, hata hivyo, anajaribu kuweka sura nzuri, kuonekana kama kiongozi wa serikali, ya umoja. Lakini baada ya dakika ishirini akashindwa kuvumilia  na kuanza kuhoji: "Mnataka nini, chaguzi tano, sita, kumi? Kura zilizorudiwa? alisikika akizungumza kwa hasira akiwaelekea wapinzani wake. Waisraeli, waliokumbwa na moja ya mzozo mbaya zaidi wa kisiasa katika historia ya nchi yao, wamepiga kura mara nne katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kuwachagua manaibu wao, lakini walishindwa kupata idadi kubwa ya kuunda serikali, hadi jana.

Muungano dhaifu

Benyamin Netanyahu ameahidi kufanyika kwa uchaguzi wa Bunge wa mara tano katika siku zijazo. Waziri mkuu wa zamani sasa ndiye kiongozi wa upinzani. Hataki kuachana na maisha ya kisiasa. Katika jumba la bunge Jumapili jioni, akiahidi kuiangusha serikali mpya ambapo alisikika akisema. "Naftali Bennett hana hadhi ya kimataifa" [kuwakilisha Israeli],

Mbele yake, muungano mpya unaotawala hautakiwi kufanya makosa. jambo ambalo laonekana kuwa ngumu kwa muungano huu wa motley wa vyama nane, ambavyo sasa vinatawala nchi. Harakati mbili kutoka kushoto, viwili kutoka katikati, vikundi vitatu kutoka kulia na kundi moja la Kiarabu, linaloongozwa na Waziri Mkuu mpya Naftali Bennett.

Anashirikiana nguvu na sentari Yaïr Lapid, ambaye atachukua hatamu za nchi katika miezi 24, kama ilivyoainishwa katika makubaliano yao ya muungano. Hadi wakati huo, Yair Lapid atakuwa waziri wa mambo ya nje wa serikali ya Kiyahudi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.