Pata taarifa kuu
MAJI-JAMII

Iran: Maandamano mengi yaibuka kufuatia ukosefu wa maji ya kunywa

Maandamano ya kupinga uhaba wa maji ya kunywa yameongezeka katika miji kadhaa magharibi mwa Iran katika siku za hivi karibuni kutokana na ukame usio na kifani unaoikumba nchi hiyo.

Katika eneo la Oroumieh, uchimbaji wa mamia ya visima virefu umekausha Ziwa Oroumieh, ziwa kubwa zaidi la chumvi nchini.
Katika eneo la Oroumieh, uchimbaji wa mamia ya visima virefu umekausha Ziwa Oroumieh, ziwa kubwa zaidi la chumvi nchini. AP - Ebrahim Noroozi
Matangazo ya kibiashara

Yote yalianza Agosti 16 katika jiji la Shahrekord. Baada ya siku kadhaa za uhaba wa maji ya kunywa, wakaazi waliingia barabarani kuandamana. "Vifo kwa maafisa wasio na uwezo," waandamanaji walipiga kelele. Hatimaye, mamlaka ilifanikiwa kuweka bomba la kupeleka maji mjini.

Lakini hali ni mbaya zaidi katika mji wa Hamedan, mji mkuu wa kihistoria wa Iran, ambao umekuwa ukikumbwa na maandamano ya kupinga uhaba wa maji kwa siku kadhaa. Hamedan, jiji lenye zaidi ya wakazi 500,000, na jimbo lake ni kitovu cha uzalishaji wa kilimo. Bwawa kuu katika eneo hilo ni kavu kabisa.

Maji ya ardhini yakauka

Uchimbaji haramu wa mamia ya visima virefu katika mkoa huo na matumizi makubwa ya maji yamesbabisha kukauka kwa maji ardhini. Mamlaka ya eneo hilo imeamua kuwalazimisha wakulima kutoa asilimia 25 ya maji kutoka kwenye visima vyao ili kuhakikisha maji ya kunywa yanapatikana kwa jiji hilo.

Katika eneo la Oroumieh, kaskazini kidogo ya nchi, hali ni kama hiyo. Uchimbaji wa mamia ya visima virefu umesababisha kukauka kabisa kwa Ziwa Oroumieh, ziwa kubwa zaidi la chumvi nchini.

Kwa miaka kadhaa, mafuriko na ukame umesababisha sehemu ya wakazi wa mikoa ya kusini mwa Iran, hasa Sistan Balochistan, kuhamia kaskazini. Ukame wa sasa nchini unatarajiwa kuzidisha hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.