Pata taarifa kuu

Vyombo vya habari vyamtaja Salman Rushdie kuwa ni "mwandishi aliyeasi"

Mamlaka ya Iran bado haijazungumzia rasmi shambulio la mwandishi Mwingereza mwenye asili ya Kihindi Salman Rushdie, huko New York, lakini vyombo vya habari vya serikali vimemtaja alman Rushdie kuwa ni "mwandishi aliyeasi".

Mamlaka ya Iran bado haijazungumzia rasmi kuhusu shambulio dhidi ya mwandishi Muingereza mwenye asili ya India Salman Rushdie.
Mamlaka ya Iran bado haijazungumzia rasmi kuhusu shambulio dhidi ya mwandishi Muingereza mwenye asili ya India Salman Rushdie. RFI / France 24
Matangazo ya kibiashara

"Shambulio dhidi ya mwandishi aliyeasi wa Aya za kishetani", limeandika shirika la Habari la serikali la IRNA au tovuti ya runinga ya serikali kwa kuzungumzia juu ya jaribio la mauaji dhidi ya Salman Rushdie wakati wa mhadhara magharibi mwa jimbo la New York, ameripoti mwandishi wetu huko Tehran, Siavosh Ghazi.

Gazeti kuu la kila siku la kihafidhina la Kayhan, limempongeza leo Jumamosi mtu aliyemdunga kisu Salman Rushdie. "Hongera kwa mtu huyu shupavu na mwenye busara aliyemshambulia muasi, katili, Salman Rushdie", limeandika gazeti hilo, ambalo mkuu wake anateuliwa na Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei. “Na tuubusu mkono wa yule aliyemdunga kisu shingoni mwa adui wa Mungu”, gazeti hilo lionaendelea.

Vyombo vya habari vyote vya Iran vimemtaja Bw. Rushdie kama "mwasi", isipokuwa Gazeti la Etemad linalotetea mageuzi. Gazeti la kila siku la Iran, gazeti la serikali, limeandika kuwa "shingo ya shetani" "imepigwa na wembe".

Vyombo vya habari vya serikali pia vimekumbusha agizo (Fatw) ya 1989 ya Imam Khomeini, mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu, ambaye alimhukumu kifo Salman Rushdie.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.