Pata taarifa kuu

Salman Rushdie alazwa hospitalini baada ya kudungwa kisu jukwaani New York

Mwandishi wa Uingereza Salman Rushdie, ambaye kitabu chake The Satanic Verses (Aya za Kishetani) kilimfanya kulengwa na agizo la Ayatollah Ruhollah Khomeini wa Iran mwaka 1989, alidungwa kisu siku ya Ijumaa alipokuwa akijiandaa kutoa mhadhara.

Mwandishi Salman Rushdie akiwa chini baada ya kushambuliwa katika Taasisi ya Chautauqua katika jimbo la New York, Ijumaa, Agosti 12, 2022.
Mwandishi Salman Rushdie akiwa chini baada ya kushambuliwa katika Taasisi ya Chautauqua katika jimbo la New York, Ijumaa, Agosti 12, 2022. AP - Joshua Goodman
Matangazo ya kibiashara

Salman Rushdie alikuwa karibu kuongea katika ukumbi wa michezo katika Taasisi ya Chautauqua wakati mtu mmoja alikimbilia kwenye jukwaa na kumpiga mwandishi na mhojiwaji wake. Picha za video zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha watu wakikimbia kumsaidia mtu aliyelala chini.

Polisi wa Jimbo la New York inasema Salman Rushdie alidungwa kisu shingoni. Alisafirishwa kwa ndege hadi hospitali ya eneo hilo. Gavana wa Jimbo la New York Kathy Hochul amefanya mkutano na waandishi wa habari na kubaini kwamba mwandishi huyo bado yuko hai. Mhojiwa amepata jeraha dogo kichwani. Mshambuliaji aliwekwa chini ya ulinzi. Uchunguzi umefunguliwa.

Mwandishi huyo, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 75, alianza kujulikana na riwaya yake ya pili ya Midnight's Children mnamo mwaka 1981, ambayo ilipata sifa ya kimataifa na Tuzo ya Uingereza ya Booker kwa kuigiza kwake India baada ya uhuru. Lakini kitabu chake The Satanic Verses kilichochapishwa miaka saba baadaye kilimsababisha kulengwa na"fatwa" ya Ayatollah Rouhollah Khomeini wa Iran ya kutaka apewe adhabu ya kifo. Riwaya hiyo ilichukuliwa na baadhi ya Waislamu kuwa haina heshima kwa Mtume Muhammad.

Salman Rushdie, aliyezaliwa mwaka 1947 huko Bombay, India, miezi miwili kabla ya uhuru wake kutoka kwa Dola ya Uingereza, anajaribu kuepuka hali kama hiyo iliyosababisha kulengwa na kashfa hii. Lakini kukuwa kwa nguvu kwa Uislamu wenye itikadi kali kusakwa na kulengwa: ishara ya mapambano dhidi ya upuuzi wa kidini na uhuru wa kujieleza. Tayari mnamo mwaka wa 2005, alizingatia kwamba "fatwa" hii ilikuwa imeunda utangulizi wa shambulio la Septemba 11, 2001.

Alilazimika kutoka wakati huo kuishi mafichoni na chini ya ulinzi wa polisi, akitoka kwenye mafichoni, alijiita Joseph Anton, kwa heshima kwa waandishi wake aliopeda, Joseph Conrad na Anton Chekhov. Ilibidi akabiliane na upweke mkubwa, ulioongezeka zaidi kwa kuachana na mkewe, mwandishi wa riwaya wa Marekani Marianne Wiggins.

Salman Rushdie ambaye anaishi New York kwa miaka kadhaa, alikuwa ameanza tena maisha ya kawaida huku akiendelea kutetea, katika vitabu vyake, kejeli na kutoheshimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.