Pata taarifa kuu
SIASA-HAKI

Iran: Kesi ya Mostafa Tajzadeh, kiongozi wa vuguvugu la mageuzi inaanza

Nchini Iran, kesi ya Mostafa Tajzadeh, kiongozi maarufu anayetetea mageuzi aliyezuiliwa tangu mwezi Julai kwa kuhujumu usalama wa taifa, imefunguliwa mbele ya mahakama ya mapinduzi mjini Tehran tarehe 14 Agosti.

Mostapha Tadjzadeh mnamo Mei 2021.
Mostapha Tadjzadeh mnamo Mei 2021. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani chini ya uongozi wa Mohammad Khatami, Mostapha Tadjzadeh ameendelea kuikosoa mamlaka katika miezi ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na ukosoaji dhidi ya Kiongozi Mkuu, Ayatollah Ali Khamenei, ameripoti mwandishi wetu huko Tehran, Siavosh Ghazi.

Mostapha Tadjzadeh ambaye ana umri wa miaka 65, alikamatwa nyumbani kwake Julai 8. Anashutumiwa hasa kwa propaganda dhidi ya serikali na njama dhidi ya usalama wa taifa. Alikataa kujibu maswali ya jaji kiongozi.

Akinukuliwa na Etemad, mke wa Mostafa Tajzadeh amebaini Jumapili hii kwamba mwanaharakati wa mageuzi "amelazimishwa kufika mbele ya mahakama".

Kukamatwa mara kadhaa

Mostafa Tadjzadeh ni sehemu ya mrengo mkali wa vuguvugu la mageuzi ambalo limezidi kujiweka mbali na mamlaka. Mostafa Tadjzadeh tayari ametumia miaka kadhaa jela. Alikamatwa mnamo mwaka 2009 baada ya ushindi ulipingwa wa rais wa zamani wa kihafidhina Mahmoud Ahmadinejad, na aliachiliwa mnamo mwaka 2016.

Tangu wakati huo, amekuwa amedai mara kwa mara kuachiliwa kwa viongozi wa vuguvugu la Kijani Kibichi, ambao wamekuwa chini ya kizuizi cha nyumbani kwa zaidi ya miaka kumi na miwili.

Kesi hii inakuja wakati kamata kamata miongoni mwa wanaharakati wa kisiasa, lakini pia watengenezaji filamu kama Jafar Panahi au Mohammad Rasoulof imeongezeka hivi majuzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.