Pata taarifa kuu
IRAN -ISRAELI USALAMA

Iran yawakamta mamluki wanaohusishwa na kundi la kijasusi la Mossad

Mamlaka nchini Iran, imesema polisi wamewakamata watu wanne akiwemo kiongozi wa matandao wa kijasusi wanaohusishwa na vitengo vya kijasusi vya Israeli.

Jiji kuu la Iran- Teheran 31 machi 2020.
Jiji kuu la Iran- Teheran 31 machi 2020. © Vahid Salemi/AP
Matangazo ya kibiashara

Iran haijataja uraia wa wanne hao japokuwa inasema kuwa watu hao walikuwa wamepokezwa mafunzo ya kuendeleza oparesheni za kijeshi na kuhujumu.

Afisi ya waziri mkuu nchini Israeli inayosimamia majasusi wake walioko nje ya nchi Mossad, imekataa kuzungumzia madai ya Iran kuwa inawazuilia wahudumu wake.

Iran na Israel hazijakuwa na uhusiano mzuri, mataifa hayo yakikabiliwa na mvutano kuhusu mpango wa nyukilia wa Iran.

Israel imekuwa ikiituhumu Iran kwa kuyauunga mkono makundi ya waasi dhidi yake, Iran nayo ikiituhumu Israeli kwa kuwauua baadhi ya maofisa wake yakiwemo mauwaji ya afisa wa ngazi ya juu wa Iran mwezi Mei. Madai ambayo Israeli haijakana wala kukubali.

Wiki iliyopita maofisa wa usalama nchini Iran walisema kuwa waliwakamata watu waliodaiwa kuwa wanaifanyia kazi Israeli ambayo waliingia nchini humo kutokea Iraq wakiwa na nia ya kutekeleza oparesheni za kigaidi.

Haya yanajiri wakati huu ambapo uhasama kati ya Iran na Israeli ukiendelea kuongezeka, Israeli ikiaapa kutumia njia zote zilizopo kuizuia Iran kuendeleza mpango wake wa kujenga kinu cha nyukilia.

Wachambuzi wa mambo wanahisi kuwa uhasama kati ya Iran na Israeli huenda ukaongezeka zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.