Pata taarifa kuu

New York Times: Israel iliamuru kuuawa kwa afisa wa jeshi la Iran

Kulingana na gazeti kuu la kila siku la Marekani la New York Times, idara ya ujasusi ya Israel ilikiri mbele ya Marekani kuwa iliamuru kuuawea kwa afisa wa jeshi la Iran, Kanali Sayyad Khodai. Kuvuja kwa habari hii kunaiweka Israeli katika hali nzito na kuongeza maradufu hasira ya Wairan.

Waombolezaji wakikusanyika karibu na jeneza la afisa wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi Sayyad Khodai wakati wa msafara wa mazishi katika Medani ya Imam-Hussein mjini Tehran Mei 24, 2022.
Waombolezaji wakikusanyika karibu na jeneza la afisa wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi Sayyad Khodai wakati wa msafara wa mazishi katika Medani ya Imam-Hussein mjini Tehran Mei 24, 2022. AFP - ATTA KENARE
Matangazo ya kibiashara

Israel bado haikiri hadharani wajibu wake wa kumuua Mlinzi wa Mapinduzi Kanali Sayyad Khodai. Lakini vyanzo vya usalama vilivyonukuliwa na vyombo vya habari havifichi kushangazwa kwao na uvujaji huo ambao uliwezesha kuchapishwa kwa habari hiyo katika Gazeti la kila siku la New York Times.

Washington yaombwa kutoa maelezo

Israel inaripotiwa kuwa inakusudia kuomba Washington ujieleza kuhusu suala hili. Uvujaji huu, inasemekana hapa, unainyooshea kidole cha lawama Israel kuwa ndiyo pekee iliyohusika na shambulio hili na kuiondolea mashtaka Marekani ambayo, Januari 2020, ilimuua Jenerali Qasem Soleimani, kamanda wa Kikosi cha Al-Quds cha Walinzi wa Mapinduzi.

Nchini Israeli, kuna hofu kwamba uvujaji huo utaimarisha nia ya Iran ya kulipiza kisasi. Kanali Sayyad Khodai aliuawa Jumapili iliyopita mjini Tehran na watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki na ambao walikimbia. Siku ya Jumanne, maelfu ya Wairani walitoa heshima zao za mwisho kwa kanali huyo, aliyetajwa kama "shujaa", na '' kuishushia lawama Marekani na Israel".

Mossad inabadilisha mfumo wake wa operesheni?

Wataalamu nchini Israel wanaeleza kuwa hayo ni mabadiliko katika mfumo wa operesheni zinazotumiwa na Mossad kwa mashambulizi ya kuvizia. Kwanza kwa sababu operesheni hiyo ilifanyika mchana na juu ya yote kwa sababu karibu waathiriwa wote wa hapo awali wa vitendo hivi walihusishwa na mpango wa nyuklia wa Iran.

Kanali Khodai alikuwa naibu kamanda wa kitengo cha 840 kilichohusika na mashambulizi dhidi ya mali za Israel duniani kote. Na hii ni ujumbe ambao Israeli inataka kutuma kwa Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.