Pata taarifa kuu

Mkutano kati ya Misri-Israel na UAE: Iran na Ukraine kwenye ajenda ya mazungumzo

Mkutano wa wakuu wa nchi tatu siku ya Jumanne umewaleta pamoja Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi, Waziri Mkuu wa Israel Naftali Bennett na Mrithi wa familia ya kifalme wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mohamad bin Zayed katika eneo la mapumziko la Bahari Nyekundu la Sharm el-Sheikh katika. Masuala mawili yametawala mazungumzo ya viongozi hao watatu: Iran na mgogoro wa Ukraine.

Rais wa Misri Al-Sissi, Waziri Mkuu wa Israel Bennett na Mwanamfalme wa Falme za Kiarabu Sheikh Mohamed bin Zayed mnamo Machi 22, 2022 huko Sharm El Sheikh nchini Misri.
Rais wa Misri Al-Sissi, Waziri Mkuu wa Israel Bennett na Mwanamfalme wa Falme za Kiarabu Sheikh Mohamed bin Zayed mnamo Machi 22, 2022 huko Sharm El Sheikh nchini Misri. VIA REUTERS - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Taarifa rasmi kutoka Misri inazungumzia kubadilishana mawazo juu ya maendeleo ya hivi punde katika masuala ya kimataifa na kikanda, anasema mwandishi wa RFI mjini Cairo, Alexandre Buccianti. Lakini imeonyeshwa kwa njia isiyo rasmi kwamba Iran ndio ambayo imewavutia viongozi watatu juu ya yote. Hasa zaidi, "tishio la kikanda ambalo linaonekana kama Tehran itatia saini, makubaliano ya nyuklia ya Iran".

Makubaliano ambayo kwa mujibu wa washiriki hayatazingatia tishio la makombora ya masafa marefu ya Iran. Mhusika mwingine mkuu wa ukanda huo, ambaye ni Saudi Arabia amewakilishwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja na Umoja wa Falme za Kiarabu. Mrithi wa familia ya kifalme, Mohammed bin Salman hivi majuzi alitangaza kwamba Israel ni "mshirika anayewezekana". Riyadh haijaelewa umuhimu wa majibu ya Marekani baada ya mfululizo wa mashambulizi ya makombora ya masafa marefu ya Iran dhidi ya ardhi yake.

Suala la mafuta

Lakini pia kumekuwa na mazungumzo ya mafuta huku mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine yakiendelea. Nchi za Ghuba, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu, zinapinga shinikizo la nchi za Magharibi la kuongeza uzalishaji na hivyo kupunguza ongezeko la bei ghafi. Lakini pia usalama wa chakula. Misri inaagiza 85% ya ngano yake na 73% ya mafuta yake ya alizeti kutoka Ukraine na Urusi.

Mkutano huu wa pande tatu ni wa kwanza wa aina yake. Misri ni nchi ya kwanza ya Kiarabu kutia saini mkataba wa amani na Israel mwaka 1979, na kumaliza hali ya vita kati ya nchi hizo mbili. Umoja wa Falme za Kiarabu, ulirejesha uhusiano wake na Israel mnamo 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.