Pata taarifa kuu

Iran: Maandamano ya kupinga ongezeko la bei ya chakula yafanyika .

Watu 22 wamekamatwa nchini Iran kwa kushiriki maandamano ya kulalamikia mfuko wa bei ya chakula katika miji miwili ya  kusini mwa taifa hilo.

Raia wa Iran akiwa dukani kaskazini mwa Tehran.
Raia wa Iran akiwa dukani kaskazini mwa Tehran. AP - Ebrahim Noroozi
Matangazo ya kibiashara

Maandamano yameonekana kwenye taifa hilo kufuatia tangazo la serikali kuwa bei mafuta ya kupika, kuku, mayai na maziwa itaongezeka kwa asilimia 300.

Tangazo la serikali ya Iran likija wakati huu ongezeko la  bei za bidhaa haswa chakula ikishuhudiwa katika mataifa tofauti duniani hali hii ikihusishwa na uvamizi wa Urusi kwa taifa la Ukraine, nchi inayotajwa kuwa msambazaji mkubwa wa chakula ulimwenguni.

Watu 15 wameripotiwa kukamatwa kusini magharibi mwa mji wa Dezful katika jimbo la Khuzestan, watu wengine 7 wakitiwa mabaroni katika mji wa Yasuj katika kaunti ya Kohgiluyeh-Boyerahmad kimedhibitisha kituo cha habari cha serikali.

Iran, inaagiza mafuta ya kupika kutoka nchini Ukraine, nchi ambayo imeathiriki kutokana na mapigano yanayoendelea ambapo wakulima wamesemekana kusitisha shughuli za ukulima kwa kuhofia kushambulia na wanajeshi wa Urusi.

Kando na Iran kuagiza mafuta ya kupika nchini Ukraine, inasemekana pia inaagiza asilimia fulani ya ngano kutoka nchini Urusi.

Hatua ya kuuza mkate wa bei rahisi kutoka nchini Iran kimagendo kwenda katika mataifa jirani ya Iraq na Afghanistan imeripotiwa kuongezeka hali ambayo imechangia katika ongezeko la idadi ya raia wanaokabiliwa na baa la njaa.

Ukame pia umetajwa kuchangia katika changamoto za kiuchumi zinazoshuhudiwa nchini Iran pamoja na vikwazo vya mataifa ya magharibi kwa nchi hiyo kutokana na mpango wake wa nyukilia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.