Usitishwaji mapigano kwa miezi miwili nchini Yemen: Ufaransa yakaribisha 'hatua muhimu'
Ufaransa imekaribisha "muhimu" wakati nchini Yemen, makubaliano ya usitishwaji vita kwa kipindi cha miezi miwili yaliyofikiwa kati ya serikali na waasi wa Houthi yanatarajiwa kuanza kutekelezwa Jumamosi hii, Machi 2 mchana, chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa. Waasi wa Houthi wako katika vita nchini Yemen kwa kipindi cha miaka minane.
Imechapishwa:
Siku ya Ijumaa Umoja wa Mataifa ulitangaza kwamba pande zinazokinzana nchini Yemen zimefikia makubaliano ya usitishwaji mapigano kwa kipindi cha miezi miwili.
"Wapiganaji wameitikia vyema pendekezo la Umoja wa Mataifa la kusitishwa mapigano kwa kipindi cha miezi miwili ambacho kitaanza kutekelezwa kesho saa moja usiku jioni," mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen Hans Grundberg amesema katika taarifa.