Pata taarifa kuu

Waandishi wawili wa habari wa kigeni wakamatwa Afghanistan

Waandishi wawili wa habari wa kigeni waliokuwa wakifanya kazi kwa niaba ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Afghanistan wamekamatwa mjini Kabul na wanazuiliwa pamoja na wenzao wa Afghanistan, shirika la Umoja wa Mataifa limesema Ijumaa wiki hii.

Zabihullah Mujahid, msemaji wa Taliban, wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Kabul mnamo Agosti 17, 2021.
Zabihullah Mujahid, msemaji wa Taliban, wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Kabul mnamo Agosti 17, 2021. AP - Rahmat Gul
Matangazo ya kibiashara

Kukamatwa huku kunafanyika karibu miezi sita baada ya Taliban kuchukuwa tena madaraka nchini Afghanistan, baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani.

"Waandishi wa habari wawili waliokuwa wkifanya kazi kwa niaba ya UNHCR na raia wa Afghanistan wanaofanya nao kazi wamekamatwa katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul. Tunafanya tuwezavyo kutatua hali hiyo", UNHCR imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, ikikataa kutoa maoni zaidi "kulingana na hali ya mambo".

Mwandishi wa habari wa kujitegemea na mwandishi wa zamani wa BBC Andrew North, ambaye amekuwa akiandika habari za Afghanistan mara kwa mara kwa miongo miwili, ni miongoni mwa mwa waandishi hao wa habari wanaozuiliwa, kulingana na mke wake Natalia Antelava. "Andrew alikuwa Kabul akifanya kazi na UNHCR akijaribu kusaidia watu nchini Afghanistan. Tunajali sana usalama wake na tunatoa wito kwa wale wote walio na ushawishi kusaidia kuachiliwa kwake," amesema.

Kwa sasa serikali ya Taliban inachunguza suala hilo, kwa mujibu wa msemaji wake, Zabihullah Mujahid.

“Tumepokea taarifa kuhusu suala hili na tunajaribu kuthibitisha iwapo wamekamatwa au la,” amesema.

Kukamatwa huku kunakuja wakati jumuiya ya kimataifa imeweka suala la uheshimishwaji wa haki za binadamu, hasa zile za wanawake, kama sharti la kurejesha uwezekano wa misaada ya kimataifa, ambayo ni takriban 75% ya bajeti ya Afghanistan.

Bila fedha hizi, na kutokana na kuzuiwa kwa mali bilioni 9.5 za Afghanistan zinazoshikiliwa nje ya nchi, Afghanistan imetumbukia katika mgogoro mkubwa wa kibinadamu. Zaidi ya nusu ya Waafghanistan milioni 38 wanatishiwa na njaa, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.