Pata taarifa kuu

Kiongozi wa Qatar apokelewa Washington na Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden amempokea, Jumatatu, Januari 31, Kiongozi wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani, mjini Washington. Katika muktadha wa mvutano kati ya Urusi na nchi za Magharibi kuhusu Ukraine, wawili hao watajadili kuhusu "utulivu wa usambazaji wa nishati ya kimataifa", Ikulu ya White House imesema. Qatar ni mshirikai mkuu wa Marekani katika masuala mengi.

Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) akimpokea, Jumatatu, Januari 31, Kiongozi wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani (kulia), mjini Washington.
Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) akimpokea, Jumatatu, Januari 31, Kiongozi wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani (kulia), mjini Washington. © AFP / Jack Guez / Chip Somodevilla
Matangazo ya kibiashara

Kwa ziara hii ya kwanza ya kiongozi wa Qatar mjini Washington tangu Rais wa Marekani Joe Biden aingie madarakani, suala la nishati litakuwa kiini cha majadiliano.

Kinachofanya ziara hii kuwa muhimu sana ni kwamba inakuja wakati mvutano kati ya nchi za Magharibi na Urusi uko juu zaidi kuhusu hali nchini Ukraine. Hatari ya uwezekano wa uvamizi wa Urusi na vikwazo vilivyokusudiwa katika kesi hii huongeza hofu ya shida za usambazaji wa gesi, na nchi za Ulaya zinapokea 40% ya gesi asilia kutoka Urusi.

Kwa vile Qatar ni mzalishaji mkuu wa gesi iliyoyeyuka, Joe Biden kwa anapaswa kuzungumzia suala hilo na Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani.

Ikiwa gesi Ulaya itakabiliwa na uhaba wa gesi, Qatar inaweza kutumika kama chanzo mbadala cha usambazaji. Nchi hii ya Ghuba ndiyo inayoongoza duniani kwa usafirishaji wa gesi asilia gesi iliyoyeyuka. Lakini mauzo yake ya nje bado yanalenga nchi za Asia.

Wawili hao pia watajadili hali nchini Afghanistan. Qatar, ambayo ina kambi kubwa ya kijeshi ya Marekani, ilikuwa na jukumu muhimu wakati majeshi ya Marekani yalipomaliza operesheni yake katika nchi hii katika masuala ya vifaa na pia katika ngazi ya kidiplomasia, kwa vile Doha inadumisha uhusiano wa zamani na Taliban ambao walitwaa tena mji mkuu wa Afghanistan mwaka jana.

Falme hiyo ilikubali kuwapokea maelfu ya wakimbizi wa Afghanistan hadi pale Marekani itakapowapa haki ya kusafiri hadi Marekani. Pia ilichukuwa nafasi ya mpatanishi katika baadhi ya mijadala na Taliban. Wiki iliyopita, msemaji wa Ikulu ya White House alieleza kuwa mkutano huu utakuwa fursa ya kuishukuru rasmi Qatar kwa usaidizi wake.

Qatar pia ni mpatanishi kati ya Marekani na Iran katika suala la nyuklia. Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar pia wiki iliyopita alikuwa ziarani mjini Tehran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.