Pata taarifa kuu
IRAN-HAKI

Benjamin Brière ahukumiwa kifungo cha miaka minane jela nchini Iran

Mahakama nchini Iran, imemhukumu miaka minane jela, Benjamin Briere,  raia wa Ufaransa baada ya kupatikana na kosa la kufanya kazi ya ujasusi nchini humo.Mawakili wake wamelaani hukumu hiyo na kusema, mashataka dhidi ya mteja wao, hayakuwa na uzito wowote.

Benjamin Brière alikamatwa mwaka 2020 kwa madai ya kufanya ujasusi nchini Iran.
Benjamin Brière alikamatwa mwaka 2020 kwa madai ya kufanya ujasusi nchini Iran. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Hukumu hii ya madai ya "ujasusi" inakuja wakati Iran na mataifa makubwa, hasa Ufaransa, yanafanya mazungumzo huko Vienna kufufua makubaliano ya nyuklia ya 2015.

Kulingana na mmoja wa mawakili wake, Benjamin Brière almehukumiwa kifungo cha miaka minane jela kwa kosa la ujasusi na propaganda dhidi ya utawala wa Iran. Pia amehukumiwa kifungo kingine cha miezi minane kwa "propaganda" dhidi ya utawala wa Iran. Ameamua kukata rufaa dhidi ya hukumu yake, wakili wake, raia wa Iran ameliambia shirika la habari la Reuters.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 36, ​​ambaye amekuwa alijitambulisha kama mtalii, alikamatwa Mei 2020 kwa kupiga "picha za maeneo yaliyopigwa marufuku" akitumia ndege isiyo na rubani ya burudani katika mbuga ya asili nchini Iran.

Benjamin Brière alianza mgomo wa kula mwishoni mwa mwezi Desemba kwa sababu mamlaka ya magereza haikumruhusu kuwasiliana na familia yake kwa simu wakati wa kuukaribisha Mwaka Mpya, amebaini mwandishi wetu wa habari huko Tehran, Siavosh Ghazi. Hukumu hii inakuja wakati mtafiti Mfaransa mwenye asili ya Iran Fariba Adelkhah, ambaye yuko chini ya kizuizi cha nyumbani tangu Oktoba 2020, amefungwa tena. Alikamatwa Juni 2019 kabla ya kuhukumiwa Mei 2020 hadi miaka mitano jela kwa kuhujumu usalama wa taifa, jambo ambalo amekuwa akikanusha kila mara.

Kuhukumiwa kwa Benjamin Brière kunakuja katika hali nyeti huku mazungumzo yakifanywa kati ya Iran na mataifa makubwa yenye nguvu ili kufufua makubaliano ya nyuklia ya 2015. Siku ya Jumatatu, waziri wa mambo ya nje wa Iran alithibitisha kwamba Iran iko tayari kubadilishana wafungwa, hasa na Marekani. Zamani Tehran ilibadilishana wafungwa na Ufaransa, Marekani na hata Australia.

Iran inawashikilia zaidi ya raia kadhaa wakiwa na pasipoti za nchi za Magharibi, wengi wao wakiwa uraia pacha, katika kile ambacho mashirika yasiyo ya kiserikali yanalaani kama sera ya kuchukua mateka iliyoundwa ili kupata makubaliano kutoka kwa mataifa ya kigeni. Wakiwa gerezani au chini ya kifungo cha nyumbani, wafungwa hao wanakabiliwa na mashtaka ambayo familia zao huona kuwa ya kipuuzi, kama vile ujasusi au kuhatarisha usalama wa taifa.

Benjamin ndiye raia wa Magharibi pekee anayejulikana aliyezuiliwa nchini Iran ambaye hana pasipoti ya Iran. Akihojiwa na RFI, dadake Blandine alionyesha hasira yake na kuomba mamlaka ya Ufaransa kuchukua hatua. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.