Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-DIPLOMASIA

Iran na Saudi Arabia zajaribu kurejesha uhusiano wao

Iran na Saudi Arabia, mataifa hasimu katika ukanda wa Mashariki ya Kati yanachukua yamepiga hatua kujaribu kurekebisha uhusiano wao baada ya miaka sita kuvunjika.

Mji wa Saudi Arabia ambapo wanadiplomasia watatu wa Iran watakuja kuhudumu katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).
Mji wa Saudi Arabia ambapo wanadiplomasia watatu wa Iran watakuja kuhudumu katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC). © Wikimedia Commons CC BY-SA 4.0 Gregor Rom
Matangazo ya kibiashara

Tehran imethibitisha kuwa wanadiplomasia watatu wa Iran wamepata viza za kusafiri hadi Saudi Arabia kuhudumu katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) yenye makao yake makuu mjini Jeddah.

"Tayari" kufungua ubalozi

"Kwa sasa, tunalenga kurejesha kazi ya wanadiplomasia wetu na OIC, lakini kama tulivyosema tuko tayari kufungua tenaubalozi wetu nchini Saudi Arabia," amesema msemaji wa Wizara ya Mmbo ya Nje ya Iran, Said Khatibzadeh.

Saudi Arabia, nchi yenye nguvu katika ukanda wa Mashariki ya Kati, ambayo viongozi na raia wao ni kutoka madhehebu ya Sunni na Iran yenye Washia wengi walivunja uhusiano wao mwezi Januari 2016 baada ya Riyadh kumuua mhubiri mashuhuri wa Kishia, raia wa  Saudi Arabaia, ambaye alisababisha kushambuliwa na kuporwa kwa ubalozi wa Saudia huko Tehran.

Mazungumzo licha ya tofauti zao

Saudi Arabia inaishutumu Iran kwa kuingilia masuala ya nchi za Kiarabu katika eneo hilo. Ufalme wa Saudi pia una wasiwasi kuhusu mpango wa nyuklia, lakini pia mpango wa Tehran wa makombora ya masafa marefu . Kwa upande wake Iran inalaani vita vilivyoanzishwa na Saudi Arabia nchini Yemen.

Licha ya tofauti hizo, nchi hizo mbili zilifanya duru nne za mazungumzo mjini Baghdad katika kujaribu kurejesha uhusiano wao. Duru ya tano imepangwa hivi karibuni katika mji mkuu wa Iraq.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.