Pata taarifa kuu

Financial Times: Saudia na Iran kufufua uhusiano wao

Maafisa wakuu wa Saudi Arabia na Iran wamekutana kwa mazungumzo ya moja kwa moja katika jaribio la kufufua uhusiano kati ya nchi hizi mbili hasimu kikanda, miaka minne baada ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kuvunjika, Gazeti la Financial Times limeripoti Jumapili hii, likinukuu maafisa katika mazungumzo hayo.

Naibu Katibu Mkuu wa Huduma ya Nje ya Ulaya (EEAS) Enrique Mora na Naibu waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi wanasubiri kuanza kwa mkutano wa Tume ya Pamoja ya JCPOA huko Vienna, Austria Aprili 17, 2021.
Naibu Katibu Mkuu wa Huduma ya Nje ya Ulaya (EEAS) Enrique Mora na Naibu waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi wanasubiri kuanza kwa mkutano wa Tume ya Pamoja ya JCPOA huko Vienna, Austria Aprili 17, 2021. © via REUTERS - EU Delegation in Vienna
Matangazo ya kibiashara

Duru ya kwanza ya mazungumzo ilifanyika  Aprili 9 huko Baghdad, ikigubikwa hasa na suala la Yemen na ilitajwa kuwa ilifanyika vizuri, Gazeti la kila siku la Uingereza limeongeza.

Maafisa wa Saudi Arabia na Iran wamejizuia kuongea kuhusu mazungumzo hayo.

Kulingana na Gazeti la Financial Times (FT), afisa mwandamizi wa Saudia amekanusha mazungumzo yoyote na Iran.

Mazungumzo haya yanakuja wakati Washington na Tehran zikijaribu kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015, ambayo Saudi Arabia ilipinga, na wakati Marekani inashinikiza kumalizika kwa mzozo wa Yemen unaoshuhudiwa katika eneo hilo, kama mzozo unaozihusisha Saudi Arabia na Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.