Pata taarifa kuu
UJERUMANI-HAKI

Ujerumani: Hukumu ya kihistoria kwa uhalifu unaohusishwa na utawala wa Syria kutolewa

Kesi ya kwanza dhidi ya maafisa wa utawala wa Syria wanaotuhumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu inamalizika Januari 13 nchini Ujerumani na kutolewa kwa hukumu.

Anwar Raslan akiwasili katika mahakama ya Koblenz, Aprili 23, 2020.
Anwar Raslan akiwasili katika mahakama ya Koblenz, Aprili 23, 2020. AFP - THOMAS LOHNES
Matangazo ya kibiashara

Mbali na kesi ya mshtakiwa, ni mfumo wa Assad wa mateso ya kimfumo dhidi ya wapinzani wake ambao utasikilizwa mahakamani. Mahakama ya Ujerumani imetoa wito wa kifungo cha maisha jela dhidi ya mshtakiwa, afisa wa zamani mwenye cheo cha kanali katika idara ya ujasusi ya Syria.

Mshtakiwa, ambaye anajulikana kwa jina la Anwar Raslan, ambaye sasa ana umri wa miaka 58, alikuwa akihudumu katika idara ya ujasusi ya Syria ambapo alikuwa mkuu wa usalama katika mji wa  Damascus na maeneo jirani ya mji huo mkuu wa nchi. Alikuwa akifanya vitendo vya ukatili katika gereza linalojulikana kwa mateso ya mara kwa mara dhidi ya wapinzani. Wale waliotumwa kufungiwa katika jela hilo walikuwa na matumaini madogo ya kutoka wakiwa hai.

Idadi ya dhuluma iliongezeka na uasi dhidi ya serikali mwanzoni mwa muongo uliopita. Anwar Raslan anatuhumiwa kwa mauaji ya watu wasiopungua thelathini na kesi 4,000 za mateso katika gereza hili la Damascus kati ya majira ya baridi 2011 na majira ya joto 2012.

Afisa huyo wa jeshi la Syria kisha akaitoroka nchi, si kwa kujutia vitendo alivyofanya bali kwa sababu alihisi kwamba kufunguliwa mashitaka kwa raia ambao hawakuwa na uhusiano wowote na upinzani hakukuwa na maana yoyote.

Ajabu ni kwamba baadaye alihamia Ujerumani na kupewa hifadhi ya kisiasa nchini humo. Akihojiwa na polisi wa Ujerumani katika faili nyingine kama shahidi, anazungumza kwa uwazi kuhusu kazi yake katika idara ya ujasusi ya Syria. Hatimaye alikamatwa pamoja na mshirika wake mwingine, aliyehukumiwa mwaka jana kifungo cha miaka minne na nusu jela kwa kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.