Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Syria: Shambulio baya dhidi ya basi laua watu wasiopungua 13 Damescus

Watu wasiopungua 13, wengi wao wakiwa wanajeshi, wameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulio la basi katikati mwa mji wa Damascus.

Picha iliyotolewa na shirika la habari la serikali ya Syria baada ya mlipuko mbaya huko Damascus, Syria, Jumatano, Oktoba 20, 2021.
Picha iliyotolewa na shirika la habari la serikali ya Syria baada ya mlipuko mbaya huko Damascus, Syria, Jumatano, Oktoba 20, 2021. AP
Matangazo ya kibiashara

Mabomu mawili yalilipuka wakati basi lililokuwa limebeba wanajeshi lilipopita chini ya daraja huko Damascus. Milipuko hiyo ilisikika sehemu kubwa ya mji mkuu wa Syria na kutikisa baadhi ya maeneo ya mji huo. Kifaa cha tatu cha kulipuka kiligunduliwa na kuteguliwa na wataalam wa kijeshi, kulingana na shirika la habari la serikali nchini Syria, SANA.

Mamlaka nchini Syria haijaeleza ikiwa shambulio hilo lilikuwa la kujitoa muhanga au bomu lililofyatuliwa kwa mbali. Picha zilizorushwa na vyombo vya habari nchini Syria zinaonyesha basi lililoteketezwa kwa moto milipuko hilo baada ya maafisa wa Zima moto kuingilia kati.

Tangu wanajeshi wa serikali ya Syria walipopata tena udhibiti wa mji wa Damescus na viunga vyake takriban miaka mitatu iliyopita, hali ya utulivu imetawala na mashambulio kama hayo ni nadra kutokea. Shambulio la mwisho lilitokea mwaka mmoja uliopita, wakati mufti wa Kisuni wa mkoa wa Damescus, Adnane al-Afyouni, alipouawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa katika gari lake. Lakini shambulio hili lilitokea huko Qoudsaya, kitongoji cha karibu cha Damescus.

Shambulio hilo la Jumatano kwa hivyo ni tukio la kipekee na ni uvunjaji wa mfumo wa usalama uliowekwa katika mji mkuu wa Syria na viunga vyake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.