Pata taarifa kuu

Jeshi la Syria lawasaka wapiganaji wa ISIS katika maeneo ya jangwani kwa msaada wa Urusi

Kikosi cha anga cha Urusi kimefanya mashambulizi kadhaa Jumatatu (Juni 14) katika jangwa la kati la Syria, ambapo wanajeshi kutoka Damascus wamekuwa wakiendesha harakati dhidi ya kundi linalojiita Islamic State tangu mapema Juni. Mapigano hayo yamesababisha maafa kwa pande zote mbili, kulingana na Kituo cha Haki za Binadamu cha Syria.

Mwanachama wa huduma za usalama wa ndani za Kikurdi za Siria zinazojulikana kama Asayish anasimama katika kizuizi cha pamoja na vikosi vya serikali ya Syria katika mji wa kaskazini mashariki wa Qamishli
Mwanachama wa huduma za usalama wa ndani za Kikurdi za Siria zinazojulikana kama Asayish anasimama katika kizuizi cha pamoja na vikosi vya serikali ya Syria katika mji wa kaskazini mashariki wa Qamishli DELIL SOULEIMAN AFP
Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha anga cha Urusi Jumatatu kimefanya zaidi ya mashambulizi 40 ya anga katika jangwa la kati la Syria kuunga mkono operesheni za jeshi la Syria dhidi ya kundi linalojiita Islamic State.

Kampeni ya wanajeshi wa serikali kuwafyeka wapiganaji imeendelea kwa siku kadhaa katika eneo kubwa kutoka eneo la kati la Homs hadi mkoa wa mashariki wa Deir Ezzor. Operesheni hizi za kijeshi, ambazo zinalenga ngome za ISIS, ambapo, kulingana na Kituo cha Haki za Binadamu cha Syria, maafa yameripotiwa pande zote mbili .

Tangu mwanzoni mwa mwezi Juni, karibu wanajeshi 30 wa Syria wameuawa katika mashambulio, kuvizia, au katika milipuko ya mabomu ya kutegwa ardhini yaliowekwa na wanajihadi.

Vita vya msituni vya kundi linalojiita Islamic State dhidi ya jeshi la Syria na washirika wake jangwani vimegeuka kuwa vita ya kutokukoma ambavyo vimesababisha mauaji ya watu zaidi ya 1,500 katika safu ya wanajeshi wa serikali na watu elfu moja upande wa wapiganaji hao wa kijihadi tangu kuanguka kwa ukhalifa uliojitangaza wa Daesh, Machi 2019.

ISIS ina maelfu ya wapiganaji, maficho ya silaha na ngome za kujificha maeneo ya jangwani.

Mkakati wake ni kulishambulia jeshi la Syria kwa kuvizia katika njia zake zote linazotumia katika usambazaji wa silaha, pamoja na barabara kuu zinazounganisha maeneo ya  kati na mashariki mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.