Pata taarifa kuu
SYRIA

UN: Mzozo umeua angalau watu 350,000 katika kipindi cha miaka Syria

Watu 350,209 waliuawa nchini Syria katika kipindi cha miaka kumi ya vita. Ni ripoti iliyosasishwa ya vita nchini Syria kulingana na Umoja wa Mataifa.

Askari wa Uturuki karibu na gari la kivita katika mji wa Syria wa Ain Issa.
Askari wa Uturuki karibu na gari la kivita katika mji wa Syria wa Ain Issa. AFP - BAKR ALKASEM
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa ulisitisha kuhesabu waathiriwa baada ya mwaka 2014, ukibaini kwamba hauwezi tena kuthibitisha habari kutoka Syria.

Hata hivyo Umoja wa Mataifa unaonya kuwa vifo ambavyo vimeshnguzwa na kuthibitishwa vimehesabiwa. Idadi sahihi ya vifo kutokana na mzozo huo bado haijulikani.

Mwanzoni mwa mzozo, mnamo mwaka 2012, ndipo vurugu zilisababisha vifo vingi. Zaidi ya watu 60,000 kwa mwaka mmoja waliuawa, bila kujua ikiwa ni wapiganaji au raia. Baada ya maka 2016 na utawala kudhibitiwa kwa mkoa wa Aleppo, idadi ya vifo ilipungua kufikia chini ya 8,000 mnamo 2020.

Mmoja kati ya waathiriwa 13 ni mwanamke. Mmoja kati ya waathiriwa 13 ni mtoto. Umojawa mataifa umehesabu tu watu ambao waliweza kutambuliwa rasmi, amesema Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Michèle Bachelet.

“Idadi hii ya wahanga 350,209 inaaminika kitakwimu. Lakini haiwezi na haipaswi kuchukuliwa kama matokeo sahihi ya mzozo nchini Syria. Badala yake, ni kikomo cha chini na kinachoweza kuthibitishwa, lakini ni hakika kwamba takwimu ya kweli bila shaka ni kubwa zaidi. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.